• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:08 PM
COVID-19: Mashabiki wa Gor Mahia tawi la Nakuru watoa msaada kwa wanaopitia hali ngumu

COVID-19: Mashabiki wa Gor Mahia tawi la Nakuru watoa msaada kwa wanaopitia hali ngumu

Na CECIL ODONGO

KUNDI moja la mashabiki wa Gor Mahia limezamia miradi ya kuwasaidia watu ambao wameathirika kimapato kutokana na janga la virusi vya corona.

Mashabiki hao chini ya tawi lao la Nakuru Prestige wamekuwa wakigawa au kusambaza vyakula kwa watu kutoka familia za kipato cha chini mjini humo

Wanaosaidiwa ni wajane, watoto na wakongwe ambao hawana njia ya kujikimu maishani.

Aidha msaada huo ambao umemfikia familia 45 unalenga wengine wengi hasa katika mitaa ya Kaptembwa, Lanet, Ronda na Bondeni kati ya mingine inayopatikana viungani mwa mji wa Nakuru.

Mwenyekiti wa Nairobi Prestige Julius Juma alieleza Taifa Leo kwamba mpango huo umekuwa ukiendelea tangu kuchipuka kwa virusi vya corona mnamo Machi.

“Tumekumbatia mpango huu kuwasaidia mashabiki wetu na wanajamii ambao wanapitia wakati mgumu kujikimu baada ya ajira yao kuathirika na COVID-19. Huu ni wakati wa kusaidiana na tunalenga kuwafikia wengi wanaohitaji msaada wetu,” akasema Bw Juma.

Poa alitoa wito kwa wahisani na wafanyabiashara mjini Nakuru waungane nao kutoa misaada zaidi ikizingatiwa mapato ya wengi yameathirika tangu kuchipuka kwa janga la corona mnamo Machi.

Baadhi ya bidhaa wanazogawa ni unga wa ugali na chapati, ndengu, maziwa na mafuta ya kupikia.

Tawi la Prestige lilibuniwa mnamo 2009 ili kuwaleta pamoja mashabiki wa Gor Mahia mjini Nakuru.

Maafisa wa Prestige na mashabiki wa K’Ogalo mara kadhaa huwakaribisha wachezaji na benchi ya kiufundi kwa kuwanunulia chamcha kila wanapofika mjini Nakuru kwa mechi za Ligi Kuu (KPL) ugani Afraha.

You can share this post!

RIZIKI: Ni mwendeshaji bodaboda aliyeacha kazi ya mama-mboga

Chifu ajengewa ofisi mpya Ngoliba

adminleo