• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 1:15 PM
Serikali ya kaunti ya Kwale yaweka mikakati kufungua biashara

Serikali ya kaunti ya Kwale yaweka mikakati kufungua biashara

Na WINNIE ATIENO

SERIKALI ya Kaunti ya Kwale imeanza kuweka mikakati kabambe ya kufungua biashara na shughuli nyingine za uzalishaji mali na ustawishaji uchumi wa eneo hilo miezi mitatu baada ya Kenya kuripoti kisa cha kwanza cha ugonjwa wa Covid-19.

Gavana wa Kwale Salim Mvurya, alisema kaunti hiyo inaendelea kunakili visa vichache vya wagonjwa wa Covid-19.

“Kufikia leo (jana Jumanne) hakuna kisa kipya ambacho tumepata,”alisema Bw Mvurya.

Alisema wagonjwa wawili walioko kituo cha Lunga Lunga wamepona na wataruhusiwa kwenda nyumbani.

Bw Mvurya alisema siku tatu zilizopita serikali ya kaunti ilipata visa tisa vya madereva kutoka Tanzania na kimoja cha dereva kutoka Malawi na wote walipeanwa kwa serikali husika.

Alisema anaunga juhudi za Rais Uhuru Kenyatta kufungua uchumi akisisitiza kuwa kamati ya Kwale imeanza kutathmini vitega uchumi katika kaunti hiyo ili siku mbili zijazo waelezee wakazi kanuni watakazofuata ili kufungua sehemu za biashara.

“Ninawahimiza wananchi tuendelee kutii kanuni na maagizo ili tuweze kudhibiti maambukizi,” aliongeza Bw Mvurya.

You can share this post!

Mmoja wa wasichana watatu waliotekwa nyara Garissa ajinasua

Afueni kwa wafanyabiashara wa Mombasa

adminleo