• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 8:55 AM
Serikali yawazia kufungua biashara Jumamosi

Na CHARLES WASONGA

KATIBU wa Wizara ya Usalama wa Ndani Karanja Kibicho anasema serikali inafikiria kufungua uchumi, japo kwa awamu, chini ya masharti mapya yatakayotangazwa Jumamosi.

Kwenye mahojiano na Redio Citizen Jumatano asubuhi Dkt Kibicho hata hivyo aliungama kuwa serikali inakabiliwa na mtihani mkubwa kuhusu suala hilo ikizingatiwa kuwa visa vya maambukizi ya Covid -19 katika siku za hivi karibuni.

“Hatuwezi kufunga nchi milele kwani serikali hupata pesa kutoka kwa kodi mbalimbali na wakati huu watu hawafanyi kazi. Binafsi nadhani tunaweza kufungua tena katika chini ya masharti makali,” akasema.

Hata hivyo, Dkt Kibicho alisema ingawa baadhi ya masharti yataondolewa, masharti ya watu kuvalia barakoa sehemu za umma na wao kutotangamana yatasalia.

Alisema kampuni ambazo zitarejelea shughuli zitahitajika kutekeleza masharti ya wafanyakazi wao kuvalia barakoa na kila mtu kutengana na mwenzake kwa umbali wa mita moja na nusu.

“Kampuni na biashara zote ambazo zitafungua sharti zizingatie masharti haya kwa sababu janga la corona lingali nasi,” Dkt Kibicho akaongeza.

Pia aliwataka Wakenya kutotarajia kurejelewa kwa maisha ya kawaida akisema hatari ya Covid-19 ingalipo na kila mmoja anahitajika kushirikiana na serikali kudhibiti athari zake.

Muda wa utekelezaji wa kafyu ya kila siku kuanzia saa moja usiku hadi saa kumi na moja alfajiri ulioongezwa kwa siku 21 zaidi unafikia tamati Jumamosi Juni 6.

Aidha, utekelezaji wa amri kutoingia na kutotoka kaunti za Nairobi, Mombasa, Kilifi, Kwale na Mandera sawa na maeneo ya Eastleigh (Nairobi) na Old Town (Mombasa) pia unapasa kumalizika siku hiyo.Na CHARLES WASONGA

KATIBU wa Wizara ya Usalama wa Ndani Karanja Kibicho anasema serikali inafikiria kufungua uchumi, japo kwa awamu, chini ya masharti mapya yatakayotangazwa Jumamosi.

Kwenye mahojiano na Redio Citizen Jumatano asubuhi Dkt Kibicho hata hivyo aliungama kuwa serikali inakabiliwa na mtihani mkubwa kuhusu suala hilo ikizingatiwa kuwa visa vya maambukizi ya Covid -19 katika siku za hivi karibuni.

“Hatuwezi kufunga nchi milele kwani serikali hupata pesa kutoka kwa kodi mbalimbali na wakati huu watu hawafanyi kazi. Binafsi nadhani tunaweza kufungua tena katika chini ya masharti makali,” akasema.

Hata hivyo, Dkt Kibicho alisema ingawa baadhi ya masharti yataondolewa, masharti ya watu kuvalia barakoa sehemu za umma na wao kutotangamana yatasalia.

Alisema kampuni ambazo zitarejelea shughuli zitahitajika kutekeleza masharti ya wafanyakazi wao kuvalia barakoa na kila mtu kutengana na mwenzake kwa umbali wa mita moja na nusu.

“Kampuni na biashara zote ambazo zitafungua sharti zizingatie masharti haya kwa sababu janga la corona lingali nasi,” Dkt Kibicho akaongeza.

Pia aliwataka Wakenya kutotarajia kurejelewa kwa maisha ya kawaida akisema hatari ya Covid-19 ingalipo na kila mmoja anahitajika kushirikiana na serikali kudhibiti athari zake.

Muda wa utekelezaji wa kafyu ya kila siku kuanzia saa moja usiku hadi saa kumi na moja alfajiri ulioongezwa kwa siku 21 zaidi unafikia tamati Jumamosi Juni 6.

Aidha, utekelezaji wa amri kutoingia na kutotoka kaunti za Nairobi, Mombasa, Kilifi, Kwale na Mandera sawa na maeneo ya Eastleigh (Nairobi) na Old Town (Mombasa) pia unapasa kumalizika siku hiyo.

  • Tags

You can share this post!

Duale apuuza jaribio la kumng’oa afisini

Hasenhuttl kusalia Southampton kwa miezi 4 zaidi

adminleo