• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 9:55 AM
Nzige watisha kuzua baa la njaa Turkana

Nzige watisha kuzua baa la njaa Turkana

SAMMY LUTTA

Wakazi wa kaunti ndogo za Turkana wanahofia njaa inayowakondolea macho baada ya mamilioni ya nzige kufaamia mashamba yao na malisho yao.

Nzige hao wanakula majani na nyasi katika maeneo ya malisho na mazao ya shambani. Wadudu hao wana rangi ya manjano, hawana mabawa na wanatembea kimakundi..

Taifa Leo ilishuhundia nzige hao wakiharibu mimea eneo la Nazarere wakulima wasiamini macho yao..

“Nimepata hasara kubwa kwa nusu ekari niliyopanda mchicha na bamia nilipangia kuvuna wiki ijayo ili niuze soko la Lowdar,” alisema Naomi Emuria.

Bi Emuria alisema kwamba nzinge hao walikula majani yote huku matikitiki maji yake yakibaki bila majani.

Bw Moses Ekutan, mfugaji, alisema kwamba mifugo wake walishikwa na ugonjwa wa kuharisha baaada ya kula mayai ya nzige hao kupitia kwa nyasi na maji.

“Kuanzia Januari uvamizi wa nzige umekuwa hatari katika kaunti yetu na italeta ukame kama hawatadhibitiwa ,”alisema Bw Ekutan.

You can share this post!

Masaibu ya chokoraa wakati wa kafyu

Zoom inavyotumika Meru kuwafaa wasiojiweza

adminleo