Kisa cha nne cha corona charipotiwa Homabay
NA GEORGE ODIWUOR
Kaunti ya Homabay imerekodi kisa chake cha nne baada ya mwalimu wa miaka 24 kuthibitishwa kuwa na virusi hivyo Jumamosi.
Mwalimu huyo wa shule ya upili ya wavulana ya Oba alitangamana na mkuu wa shule hiyo aliyefariki Jumatatu kutokana na virusi vya corona.
Kutokana na habari zilizotolewa na kaunti hiyo mgonjwa huyo alihudhuria mkutano uliwekwa na a mkuu wa shule hiyo Mei 19 huko Rachuonyo Mashariki.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na walimu wengine wanne pamoja na afisa kutoka kitengo cha fedha.
Wakati wa mkutano huyo hakuna aliyejua kwamba alikuwa na virusi hivo. Inasemekana kwamba mkuu huyo wa shule alienda nyumbani kwake kaunti ya Migori baada ya kutembelea mji wa Oyigis Rachuonyo kusini
Aliripoti kwanza alikuwa hajihisi vivuri baada ya kufika nyumbani Migori.
Mwalimu huyo mkuu alitafuta matibabu kwenye hospitali zilizokuwa karibu baada ya kuzidiwa na kupelekwa kwenye hospitali ya Agha Kan Kaunti ya Kisumu na akakosa kuhudumiwa kwa sababu ya kukosa bima ya afya.
Hapo ndipo alipelekwa tena kwenye hospitali ya kibinafsi hapo Kisumu lakini akaaga dunia kabla ya kuhudumiwa na daktari.