Habari Mseto

Watu 6 wauawa katika mapigano ya Narok

June 7th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

NA GEORGE SAYAGIE

Maafisa wa usalama wamesema kwamba mapigano ya kikabila yanayoendelea kati ya jamii za mpaka wa Narok na Nakuru yameacha watu 6 wamefariki na watu 13 na majeraha.

Machafuko hayo kati ya jamii hizo mbili yalioanza Jumamosi katika Kijiji cha Oloruasi na Olpusimoru na Kijiji cha Ololoipangi Jumapili zimeacha familia nyingi bila makao huku nyumba zaidi ya 20 zikichomwa.

Kufuatia mapigano hayo, viongozi wa eneo hilo walifanya mkutano Jumanne katika afisi ya kamishna wa kaunti ya Narok Samuel Kimiti uliohudhuriwa na Gavana wa Narok Samuel Tunai na Mbunge wa Narok Kusini Korein Lemein..

Vita hivyo vilianza baada ya wizi wa ng’ombe katika Kijiji cha Oloruasi, Bw Kimiti alisema.

“Tumegundua kwamba kuna mengi zaidi ya wizi wa mifugo na viongozi lazima wakome kuchochea wananchi,” alisema Kimiti.

Polisi wamewakamata watu 9 kutoka kaunti ndogo ya Kuresoi kuhusiana na vita hio Olpusimuru Narok Kusini.

Msimamizi huyo alisema kwamba kuna wanasiasa wanaofanya mikutano na wananchi na kuwachochea kupingana..