Habari Mseto

Diwani pabaya kwa kukosa vikao 11 vya bunge la kaunti

June 9th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

NA COLLINS OMULO

Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kaunti ya Nairobi Abdi Nguyo amesimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge hilo baada ya kukosa kuhudhuria vikao mara 11 mfululizo.

Hii inajiri huku vita dhidi ya madiwani wa chama ya Jubilee vikiendelea.

Kufuatia kusimamishwa, kwake diwani huyo wa Matopeni Springs Valey alisema kwamba atafika kortini kupiga maamuzi hayo ya bunge hio ya Nairobi.

Spika wa bunge hio Beatrice Elachi alitaja hayo alisema kwamba Bw Guyo hatoendelea kufurahia huduma  ambazo amezoea kwa miezi atakayokuwa nje ya bunge.

Bi Elachi alisema kwamba maamuzi hayo hayahitaji kutathiminiwa na mamlaka yeyote huku akiangiza afisi ya karani pamoja na afisi ya afisa wa usalama bungeni kuhakikisha kuwa maamuzi hayo yametekelezwa.

Kusitishwa kwa Bw Guyo kulifuatia kupitishwa kwa kamati iliyokuwa ikichunguza madai kwamba madiwani wa chama cha Jubilee hawakuwa wanahudhuria vikao, iliyoanzishwa na diwani mteule Mary Ariviza hapo Machi 6 ,2020.

Kamati hiyo inayoogozwa na spika wa bunge hilo iligundua kwamba Bw Guyo alikuwa amekosa kuhudhuria vikao 11 mfululizo kati ya Januari 9 na Mechi 9, 2020 hiyvo alikiuka sheria ya bunge ya 242.

Sheria hiyo inasema kwamba diwani akikosa kuhudhuria vikao vya mbunge kwa mara nane bila ruhusa kutoka kwa spika, spika ataripoti kisa hicho kwa bunge na kamati hiyo itasikiza kesi hiyo. Ripoti hiyo ilionyesha kwamba Bw Guyo hakumwandikia spika kumweleza kwanini hakuwa anahudhuria vikao.