Watu 4 zaidi wauawa Marsabit
NA JACOB WALTER
Watu wanne zaidi waliuawa katika Kaunti ya Marsabit kwenye vita vipya vilivyanzishwa na majambazi waliojihami kwa bunduki.
Vita hivyo vya Jumamosi viliendelea licha ya wito wa kusitisha machafuko kutolewa na serikali.
Wanne hao waliuawa huku maafisa wakuu wa eneo hilo wakipata ajali ya ndege katika kaunti ya Meru wakielekea Marsabit ili kusuluhisha mgogoro kati ya jamii hizo mbili.
Tukio hilo lilitokea wadi ya Kokuto, Sagante-Jaldesa Marsabit ya kati Jumamosi jioni.
Kamanda wa polisi wa Marsabit ya kati Benjamin Mwathi alisema kwamba wanne hao walipiga risasi na majangili wasiojulikana waliojihami walipokuwa wakipeleka mifung’o Jaica kunywa maji.
“Tumepoteza wafungaji wengine wanne Kokuto walipokuwa wakipeleka ngombe kukunywa maji,” alisema Bw Mwathi.
Watu zaidi ya 20 wanahofiwa kuwa wamefariki kati ya muda wa wiki moja katika mauaji ya kinyama yanyo ekelezwa na watu wasiojulikana.
Watu wanne waliuwawa Juni 6 Bdandero katika kaunti ndogo ya Moyale ktika wizi wa ng’ombe ulioelekea vita kati ya jamii za Borana na Degodia katika mpaka wa Marsabit-Wajir.