Wanasiasa wanaochochea ghasia waonywa
NA BRUHAN MAKONG
Serikali imeonya wanasiasa kutoka kaskazini mwa nchi dhidi ya kuchochea vita kati ya jamii zinazoishi kwenye mpaka wa Marsabit na Wajir.
Vita hivyo vilivyoanza siku chache zilizopita imeacha watu wasiopungua tisa wakiwa wamefariki na watu wengine 200 bila makao.
Walitoroka makwao wamepiga kambi katika maeneo ya Basir, kaunti ndogo ya Eldas baada ya vita kuzuka.
Watu wanne zaidi wamepotea na hawapatikani waliko kufuatia vita dhidi ya mahala pa malisho kati ya jamii za Degodia na Borana Sololo kaunti ya Marsabit.
Serikali ilionya kwamba atayepatikana na kuhusika na vita hivyo watachukuliwa hatua kali.
Akiongea katika mkutano wa kurejesha amani katika Kijiji cha Badan-Rero kamishna wa eneo hilo la Kaskazini Mashariki Nicodemus Ndalana alionywa wnasiasa dhidi ya kuingiza wananchi wasio na hatia katika vita kwa tamaa ya kujitafutia umaarufu wa siasa.
“Kama kuna wahalifu waohusika na mauji haya, naomba sana wanasiasa wasiwe wamehusika, ni rahisi sana sisi serikali kuwakamata,” alionya Bw Ndalana.