• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 10:55 AM
FUNGUKA: ‘Waume singo ni matapeli wa mapenzi, nataka waliooa’

FUNGUKA: ‘Waume singo ni matapeli wa mapenzi, nataka waliooa’

Na PAULINE ONGAJI

BAADA ya kulaghaiwa mara kadhaa katika mahusiano na hata ndoa, Annah, 32, ameamua kutojihusisha na madume wasio na wake.

Annah ni mrembo ajabu na kusema kweli yeye ni mmojawapo wa mabinti ambao wakijitokeza, wanaacha watu – wake kwa waume – wakipindua vichwa vyao.

Anafanya kazi ya uhasibu katika shirika moja la kimataifa lenye afisi zake jijini Nairobi.

Pia, yeye ni mama wa watoto wawili na ameolewa na kutaliki mara mbili.

Anasema kwamba udanganyifu kwa upande wa wanaume, ndio ulisababisha ndoa zake mbili kufeli, na hii imemfanya kuchukua maamuzi ya ajabu katika mahusiano, kama anavyosimulia.

“Nimeamua kuchumbiwa na wanaume walio na wake sio kwa minajili ya kuharibu ndoa za watu, lakini ni kwa sababu nahisi kwamba wanaume hawaaminiki na wote ni wadanganyifu.

Naamini kwamba wanaume waaminifu hawapo, sina haja ya kuchumbiwa na wanaume wasio na wake watakaoahidi mengi, kisha baadaye kukulaghai.

Nafanya hivyo kwa sababu najua hakuna mwunganisho wowote na mwisho wa siku ataenda nyumbani kwa mkewe, hivyo hakuna hisia zozote za mapenzi.

Kwa upande mwingine, nikianza kuchumbiana na waume za watu hakuna haja ya kujifanya kujawa na mapenzi ili uhusiano udumu.

Hata hivyo, haimaanishi kwamba sijikakamui kuhakikisha kwamba nitafurahia tukiwa pamoja wakati wa mahaba.

Niko tayari kumuandalia chakula kizuri, kumkanda, kumchemshia maji ya kuoga na kumfurahisha vilivyo wakati wa mahaba, ili pia mimi niridhike.

Lakini kwa kawaida simruhusu mume wa mtu kulala kwangu, na sina haja na pesa zake.

Ikiwa kaka atanihudumia vyema katika awamu hii basi inamaanisha kwamba amepita mtihani na pengine atafuzu kuandamana nami likizoni ng’ambo kwa burudani zaidi.

Niko tayari kumlipia likizo ghali hata ng’ambo kufurahia pamoja, lakini tukirejea afahamu kwamba kwangu hakuna nafasi ya mwanamume, arejee kwa mkewe.

Ikiwa wewe ni mume wa mtu na una haja ya mahaba bila mwunganisho, basi mimi nitakufaa sana.

Ukiwa nami usiwe na wasiwasi kwamba nitakutumia jumbe za mapenzi, wala kuhitaji uangalifu wako, au hata kujaribu kuwasiliana na mkeo.

Ukiwa nami, nitakuhakikishia usalama wa uhusiano au ndoa yako.

Nilipokuwa nikikua niliamini kwamba kuna penzi halisi na kujitolea, lakini hata hivyo nilipozidi kukomaa kiumri, nilianza kuamini kwamba hiyo ilikuwa ndoto tu.

Nilipokuwa msichana nilishuhudia babangu akimlaghai mamangu kila wakati.

Mamangu alivumilia kuvunjwa moyo katika ndoa.

Ni kutokana na sababu hii ndipo nilijiambia katu siwezi kuvumilia katika uhusiano au ndoa iliyojaa udanganyifu.

Mahusiano siku hizi hayaeleweki kwa sababu watu sio wakweli na siamini kwamba kuna mwanamume yeyote mwaminifu.

Ni mkondo ambao wanawake wote wanapaswa kufuata ikiwa wanataka kuishi kwa amani.

Wasivumilie katika mahusiano ambayo wana uhakika kwamba watalaghaiwa hatimaye, na katika harakati hizo wasijinyime burudani ya mahaba.”

You can share this post!

Kibwana atangaza kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2022

UMBEA: Mke, elewa nafasi yako katika ndoa sio kujibeba kama...

adminleo