• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 5:46 PM
Changamoto serikali ikipanga kurejelewa kwa masomo

Changamoto serikali ikipanga kurejelewa kwa masomo

NA KITAVI MUTUA

Serikali inajizatiti kusaka mbinu mwafaka kuhakikisha wanafunzi wataweza kuweka umbali wa mita moja darsani shule zikifunguliwa.

Prof Magoha alisema kwamba wataalamu wa Wizara ya Afya walishauri serikali kuwa madarasa yenye wanafunzi zaidi ya 45 yanapaswa kupunguzwa wanafunzi ili kupunguza kusambaa kwa virusi vya corona.

“Tumeshauriwa na Wizara ya Afya kwamba darasa moja linapaswa kuwa na wanafunzi kati ya 15 na 20. Nyote mnajua kwamba hii itakuwa ngumu kwa sababu shule hazina madarasa ya kutosha,” alisema.

Kenya ina wanafunzi milioni 24 wa shule ya msingi na shule ya upili na umbali wa mita moja inamaanisha kwamba wanafunzi milioni 15 watalazimika kusaka mbinu zingine za kusoma.

Kuna baadhi ya shule za mjini ambazo zina zaidi ya wanafunzi 70 katika kila darasa huku walimu wote nchini wakiwa 130,000.

Tafsiri: Faustine Ngila

You can share this post!

Jambazi sugu aliyeachiliwa kimakosa asakwa

Kiunjuri azindua chama kipya

adminleo