• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 6:50 AM
Butwaa na majonzi wanne wakifariki kijijini

Butwaa na majonzi wanne wakifariki kijijini

NICHOLAS KOMU na FAUSTINE NGILA

Wakazi wa kijiji cha Kiamwathi Kaunti ya Nyeri walipigwa na butwaa na majonzi kufuatia kuuawa kwa watu watatu na mtu mwingine kujitia kitanzi usiku.

Mtu mmoja aliumia huku mwanaume anayekisiwa kuhusika na mauaji hayo akijitia kitanzi.

Watu watatu waliuliwa huku mwingine akijitia kitanzi katika visa viwili tofauti vilivyoripotiwa kwenye boma mbili tofauti zilizo na umbali wa mita 300.

Kisa cha kwanza kilitendeka mwendo wa saa nne usiku ambapo mwanaume wa miaka 82 alikatwa na panga hadi kifo alipokuwa akipigana na mpwa wake kuhusiana na pesa za wazee zinazopeanwa na serikali.

Polisi walisema Bw Elijah alikatwa kwa panga mpaka akafriki na mpwa wake Dancun Macharia 41 walipokuwa wakipingania pesa ambazo idadi yake haikujulikana.

Mzee huyo iliripotiwa kwamba alimlaumu mpwa wake kwa kumuibia pesa aliyopokea kutoka kwa serikali kupitia kwa programu ya serikali ya kuwapa wazee pesa.

Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Nyeri ya Kati Paul Kuria alisema kwamba mzee huyo alikabiliana na mpya wake kuhusiana na madai kwamba aliiba pesa vilivyozua vita ya mapanga.

“Alichukua panga na kuamua kukabiliana na mpwa wake nyumbani kwake. Mshukiwa naye akachukua panga ili kujilinda na panga iliyopelekea vita ya mapanga kati ya wawili hao hapo ndipo alimshinda nguvu na kumkata mwanaume huyo hadi kifo,” alisema Bw Kuria.

Baada ya kumuua alikimbia kujificha kwa shamba lake huku akiwa na maumivu.

Polisi waliitikia wito huo huku wakimkamata Bw Macharia na kumpeleka hospitalini kabla ya kumpeleka kortini.

“Mshukiwa huyo alikuwa amekatwa kichwani na sasa ako sawa tumemzuilia kabla ya kumpeleka kortini,” mkuu wa polisi alisema.

You can share this post!

Ujangili na al-Shabaab vikwazo kwa utalii Garissa

Messi afikisha mabao 700 kitaaluma Barcelona wakiambulia...

adminleo