Habari Mseto

Zaidi ya wasichana 5000 watungwa mimba Meru

July 1st, 2020 Kusoma ni dakika: 1

DAVID MUCHUI na FAUSTINE NGILA

Wasichana 170 wenye umri wa kati ya miaka 10 na 14 wamepata uja uzito kaunti ya Meru kati ya Januari na Juni.

Hii ni kati ya wasichana 5,270 ambao wana ujauzito wanaorekodiwa kwenye mfumo wa habari za afya.

Habari hizo zinaonyeshwa kwamba wasichana 5,100 wa miaka kati ya 14 na 19 wana ujauzito kaunti ya Meru.

Kaunti ndogo ya Imenti Kaskazini imeogoza na wasichana wajawazito 80 ikifuatiwa na Imenti Kusini na 31.

Kulingana na data ya hospitali Igembe Kusini inaidadi kubwa zaidi na 979 ikifuatiwa na igembe ya kati 978 na Igembe Kaskazini 823.

Wengine Imenti Kusini 587, Imenti Kaskazini 44o, Tigania Magharibi 412, Imenti ya kati 310, Tigania ya kati 256, Buuri Mashariki 230, Buuri Magharibi 112.

Ripoti iliyotolewa na Wizara ya Elimu mwaka uliopita ilionyesha kwamba Meru iliongoza kwa Mimba za wasichana wa umri mdogo.

“Tumeunda klabu ya akina mama wenye umri mdogo katika hospitali za kaunti ngogo za Mikinduri, Kangeta, Nyambene, Muthara na Mutuati ambapo kina mama wenye umri mdogo ukutana kwa ushauri.

“Tuligundua kwamba wasichana wadogo ukataliwa na jamii baada ya kupata ujauzito, hio inaelekea kuzitia kitanzi,” alisema Doris Muriuki mratibu wa maswala ya afya Meru.