Uagizaji wa sukari kutoka nje wapigwa marufuku
GERALD ANDAE na FAUSTINE NGILA
Wizara ya Afya imepiga marufuku uagizaji wa sukari kutoka nchi za nje na utoaji wa vyeti vya kufanya biashara.
Hii ni njia ya kuondoa sukari wa bei rahisi sokoni ambao unawaathiri wakulima humu nchini.
Waziri wa Kilimo Peter Munya alisema uagizaji wa sukari hiyo umeathiri wakulima humu huku bidhaa zao zikikosa soko .
Bw Munya alisema wizara hiyo iligundua kwamba bidhaa hizo zilikuwa zinaingia nchini kupitia mpaka wa Busia huku wanabiashara wakora wakitumia masaa ya kafyu kuziingiza humu nchini.
“Tumesitisha kuagizwa kwa sukari kutoka nchi za nje haraka iwezekanavyo. Pia tumesitisha vyeti vya kuagiza sukari nje kwa muda ,” alisema.
“Kuagiza kwa sukari kutoka nje kumefanya sukari ya Kenya kukosa soko.Huku tani moja ya ikiwa inatoka Sh85,260 ukilinganisha na bei ya CIF ambayo ni Sh60,117 na zote ni kiasi sawa,” akasema.