• Nairobi
  • Last Updated April 16th, 2024 6:55 PM
Wengine 637 wapatikana na corona, 10 wafariki

Wengine 637 wapatikana na corona, 10 wafariki

Na CHARLES WASONGA

WATU wengine 637 wamethibitishwa kuwa na virusi vya corona nchini Kenya, kulingana na takwimu zilizotolewa na Waziri Msaidizi wa Afya Rashid Aman.

Idadi hiyo imefikisha 14, 804 visa vya maambukizi ya janga hilo kufikia Jumatano, Julai 22, 2020.

Dkt Aman alisema kuwa wagonjwa hao wapya, 361 wa jinsia ya kiume na 276 wa jinsia ya kike, walipatikana baaa ya jumla ya sampuli 4, 275 kupimwa ndani ya muda wa saa 24.

“Kwa hivyo kufikia sasa (Jumatano) idadi jumla ya sampuli ambazo zimepimwa ni 254, 273 tangu kisa cha kwanza kuripotiwa nchini,” akaeleza.

Dkt Aman aliongeza kuwa jumla ya wagonjwa 10 wamefariki kutoka na Covid-19 huku wengine 499 wakipata afueni.

Visa hivyo 637 vipya vya maambukizi vimesambazwa katika kaunti kwa njia ifuatayo; Nairobi inaongozwa kwa kuandikisha visa 342, Machakos (85) Kajiado (57), Kiambu (51), Nakuru (22), Mombasa (17), Marsabit(15), Nyeri (13), Busia (10), Murang’a (9), Uasin Gishu (6), Bomet (5), Kericho (3), Kisii (3) na Marsabit (2).

Kaunti za Narok, Vihiga, Meru, Garissa, Embu, Kakamega, Kisumu Kitui, Laikipia, Kilifi na Homa bay zimesajili kisa kimoja kila moja.

Katika kaunti ya Nairobi visa 342 vimesambazwa kama ifuatavyo; Westlands (32), Kamukunji (44), Langata (31), Embakasi Kusini (26), Dagoretti Kaskazini (24), Embakasi Mashariki (24), Kasarani (23), Embakasi Magharibi (19), Kibra (18), Makadara (17), Starehe (17), Ruaraka (14), Emabakasi ya Kati (13), Embakasi Kaskazini (11), Roysambu (11). Mathare (10) huku Dagoretti South ikisajili visa vya vinane (8).

You can share this post!

WASONGA: Wizara itoe fedha kwa shule kulipa wafanyakazi

Serikali yasema mawaziri hawajazimwa kuzuru mashinani

adminleo