• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 3:25 PM
Maafisa wachunguza visa vya mauaji ya wazee Kwale

Maafisa wachunguza visa vya mauaji ya wazee Kwale

Na MISHI GONGO

IDARA ya usalama Kaunti ya Kwale inachunguza visa vya mauaji ya wazee watatu waliouawa katika hali ya kutatanisha ndani ya muda wa wiki tatu.

Kulingana na kamanda wa polisi kaunti hiyo Bw Joseph Nthenge, wazee watatu wa kati ya umri wa miaka 60 hadi 80 waliuawa kwa kukatwakatwa mapanga katika mazingira tatanishi Matuga, Lungalunga, na Kinango.

“Ndani ya muda wa wiki tatu tumepoteza wazee watatu katika hali tatanishi. Uchunguzi umeanzishwa na yeyote atakayepatikana kuhusika na mauaji hayo atachukuliwa hatua kali,” akasema.

Nthenge ameelezea kusikitishwa kwake na jinsi visa vya kuwatoa uhai wazee vinavyochipuka upya hata baada ya idara ya usalama kuingilia kati na kukomesha visa hivyo.

“Visa vya wazee kutolewa uhai tulikuwa tumevikomesha, lakini tunashangaa sasa vimerudi tena. Hatutapumzika hadi tuhakikishe kuwa visa hivi tumevimaliza,” akasema.

Vilevile Nthenge ameionya jamii dhidi ya kusuluhisha mizozo ya kijamii kwa kuchukua hatua mikononi mwao kwa kutekeleza mauji hasa mizozo ya ardhi kwani mkono wa sheria hautawasaza.

You can share this post!

Muguna kugura Gor

VINYWAJI: Jinsi ya kutayarisha sharubati ya tikitimaji

adminleo