• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 3:23 PM
USHAURI: Ukihisi maumivu ya kichwa unafaa kufanya nini?

USHAURI: Ukihisi maumivu ya kichwa unafaa kufanya nini?

Na MARGARET MAINA

[email protected]

KICHWA kikikuwanga, unaweza kufanya mambo kadhaa kama vile;

• achana na mawazo

• epuka vilevi vyote

• oga/ koga maji ya moto

• kula vyakula vya asili

• kuwa mtulivu

• pata kupumzika

• kunywa maji ya kutosha kila siku

• epuka vyakula kama siagi ya karanga, chokoleti, chai ya rangi, kahawa na soda

• tumia zaidi vyakula vyenye Vitamini C, Vitamini B2 na madini ya magnesium

• fanya masaji ya kichwa, ya shingo na ya mgongo

• sikiliza muziki uupendao

Vilevile unaweza pia kutumia vitu vinavyopatikana nyumbani

Kumbuka maumivu yakizidi muone daktari kwa uchunguzi zaidi.

Shurubati ya mnanaa

Dawa nyingine ya asili ya kutibu maumivu ya kichwa ni juisi ya mnanaa kwa kuwa mnanaa una vitu vya kutoa maumivu ya kichwa vijulikanavyo kama ‘menthol’ na ‘menthone’.

Pia unaweza kutumia mvuke uliotokana na chai ya majani ya mnanaa ujifunikie sehemu ya mbele ya kichwa chako.

Tangawizi

Inachofanya tangawizi ni kupunguza maambukizi kwenye mishipa yako ya damu.

Kuna namna mbili unaweza kutumia tangawizi kutibu maumivu ya kichwa.

Moja ni kutengeneza juisi ya tangawizi, kipande kidogo tu cha tangawizi tumia maji na blenda tengeneza juisi yake upate kikombe kimoja na uchuje kisha ongeza vijiko vikubwa viwili vya juisi ya limau na asali kidogo na unywe .

Namna ya pili ni kutengeneza chai ya tangawizi ukitumia tangawizi, maji na asali

Kunywa chai hii.

Unaweza pia kutafuna kipande kidogo cha tangawizi kupunguza maumivu hayo.

Kipande cha barafu

Kipande cha barafu kinasaidia kupunguza muwako au joto vitu ambavyo ni moja ya vitu vinavyoweza kusababisha maumivu ya kichwa.

Barafu pia ni nzuri kurekebisha hali ya maumivu.

Kwanza weka kipande cha barafu katika kitambaa kisafi na uweke nyuma ya shingo yako kwa dakika kadhaa.

Namna nyingine ni kuweka kitambaa safi ndani ya maji ya baridi sana kama barafu kisha funika sehemu ya mbele ya kichwa chako na kitambaa hiki kwa dakika tano.

Siki ya tufaha

Tunda lenyewe na hata siki yake vinaweza kutumika kutuliza maumivu ya kichwa sababu ya uwezo wake wa kuweka usawa alkalini kwenye mwili wako.

Siki ya tufaha (Apple cider vinegar) inatumika na watu wengi duniani kama dawa ya asili kutibu maumivu ya kichwa.

Ongeza kijiko kidogo kimoja cha siki ya tufaa ndani ya maji kikombe kimoja na unywe kwa siku kadhaa kutibu maumivu yako ya kichwa.

Limau

limau inayo sifa ya kukufanya mtulivu kwa asili kabisa bila madhara yoyote .Limau linaondoa asidi iliyozidi mwilini pia lina vitamini C.

Kamua maji ya limau kisha changanya na maji fufutende kikombe kimoja na unywe yote kwa siku kadhaa.

Mdalasini

Mdalasini hutumika kutibu maumivu ya kichwa hasa yale yaliyotokana na hewa ya baridi.

Chukua unga wa mdalasini kiasi cha kijiko kikubwa kimoja, ongeza maji kidogo kupata mkorogo mzito kisha paka kwenye kipaji cha uso na uache hapo kwa dakika 30 hivi kisha jisafishe kwa kutumia maji safi.

Chai ya kijani (Green Tea)

Chai ya kijani inaweza kukuondolea maumivu ya kichwa sababu inayo viondoa sumu ambavyo vinaweza kusaidia kuondoa maumivu ya kichwa moja kwa moja.

Maji ya kunywa

Mara nyingi watu wanaosumbuliwa na maumivu ya kichwa wengi wao huwa ni wale wasiotilia mkazo suala la kunywa maji mengi ya kutosha kila siku.

Hali ya kichwa kuwa na maumivu inaweza ikawa na tafsiri mbili tu; ama sumu zimezidi au asidi ambayo nayo ni kama sumu au taka za mwili, vimezidi mwilini. Ni vitu ambavyo vinaweza kuondolewa kirahisi kwa kutumia maji ya kunywa tu.

Unaposikia maumivu ya kichwa chukua maji mara moja na unywe na hutakawia kuona mabadiliko mazuri.

You can share this post!

ODM yakanusha madai Raila amesaliti Pwani

CORONA: Watu 23 wafariki

adminleo