• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Ripoti kuhusu maandalizi ya corona iandaliwe -Mahakama

Ripoti kuhusu maandalizi ya corona iandaliwe -Mahakama

Na RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA kuu Jumatatu ilikataa kufutilia mbali agizo la kuitika Serikali iwasilishe ripoti jinsi imejiandaa kuzuia na kupambana na ugonjwa wa Corona.

Hata hivyo, Jaji James Makau alisema ripoti iliyowasilishwa mahakamani na Wizara ya Afya kuhusu maandalizi ya kupambana na ugonjwa huu yaridhisha.

Jaji huyo alisema serikali haikuathiriwa na agizo hilo iliyoombwa na Chama cha Wanasheria nchini-LSK.

Jaji Makau alisema madai kwamba mawaziri wa afya , mashauri ya kigeni, uchukuzi na usalama wa ndani hawakupewa fursa ya kujitetea.

“Kesi iliyowasilishwa mnamo Aprili 8,2020 iliwasilishwa baada ya agizo kutolewa Machi 6 na 18 2020 ikiitaka Serikali iwasilishe ripoti hiyo ya maandalizi,” alisema Jaji Makau.

Wizara za afya, uchukuzi, masuala ya kigeni na usalama wa ndani zililalamika kuwa maagizo yaliyotolewa na mahakama yalikiuka mwongozo wa usimamizi wa idara za serikali.

Wizara hizo ziliomba korti ifutilie mbali maagizo hayo lakini Jaji Makau akakataa akisema ugonjwa wa Corona umehatarisha maisha ya wengi.

Jaji huyo alisema ombi la wizara hizi kufutilia mbali maagizo ziwasilishe kortini ripoti ya Covid-19 liliwasilishwa mahakamani baada ya siku 40.

Alisema hakuna sababu zilizotolewa na wizara hizo sababu ya kuchelewa kuwasilisha ripoti na ushahidi kortini.

“Hakuna sababu zozote zilizotolewa zikieleza za kuchelewa kuwasilisha majibu ya kesi ya LSK na madaktari wawili,” alisema Jaji Makau.

You can share this post!

Serikali yashangaa bado mikusanyiko ya umma inafanyika

Hatutakubali ushoga wala usagaji hapa Kenya – Kinuthia

adminleo