• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 8:50 AM
Hakuna ulegevu ndani ya ODM – Mbadi

Hakuna ulegevu ndani ya ODM – Mbadi

CHARLES WASONGA

MWENYEKITI wa ODM John Mbadi amekana madai kuwa chama hicho kilikosa uongozi na mwelekeo wa pamoja wakati Raila Odinga alipokuwa akipumzika baada ya kufanyiwa upasuaji Dubai.

Mbunge huyo wa Suba Kusini alisema hali iliyodhihiriki katika Seneti ambapo maseneta wa chama hicho walichukua misimamo tofauti katika suala la ugavi wa fedha miongoni mwa kaunti haifai kufasiriwa kuwa ODM ilikosa msimamo.

“ODM imekuwa chama thabiti hata wakati huu ambapo Jakom (Raila) ameshauriwa na madaktari kwamba apumzike. Suala la ugavi wa fedha katika kaunti liliendeshwa na maseneta kwa misingi ya wangeongezewa fedha na wale ambapo wangepoteza. Hii ndio maana maseneta wa ODM hawakupiga kura pamoja,” Bw Mbadi akaambia Taifa Leo Jumatatu kwenye mahojiano kwa njia ya simu.

Mbunge huyo ambaye ni kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa alikuwa alikuwa ajibu madai ya Wakili Mkuu Ahmednassir Abdullahi aliyenukuliwa magazetini Jumapili akisema ODM imeonakana kukosa uongozi na mwelekeo wakati huu ambapo Bw Odinga anapumzika.

“Bila Raila ODM inaonekana chama chama ambacho kimekosa uongozi. Hali hii ilionekana katika Seneti Jumanne wiki jana wakati wa mjadala kuhusu ugavi wa fedha pale mgawanyiko miongoni mwa maseneta wake ulichangia kuangushwa kwa mfumo uliopendelewa na Rais Uhuru Kenyatta,” Bw Abdullahi akasema.

Ni maseneta wa wanne kutoka Luo Nyanza wakiongozwa na kiongozi wa wachache James Orengo ndio waliunga mkono hoja iliyopendekezwa na Kiranja wa Wengi Irungu Kang’ata. Wengine walikuwa; Ochilo Ayacko (Migori), Fred Outa (Kisumu) na Moses Kajwang (Homa Bay).

Lakini wengine kama vile Ledama Ole Kina (Narok) na Okong’o Omogeni (Nyamira) waliounga na mwenzao sita kutoka Pwani kwa kupinga mfumo huo kwa misingi kuwa itapelekea kaunti zao kupokonywa fedha nyingi.

Lakini jana, Mbadi alisema misimamo tofauti iliyochukuliwa na maseneta wa ODM kuhusu suala hilo haifai kuchukuliwa kuashiria kuwa kuna uasi ndani ya chama hicho.

“Maseneta wetu kutoka Pwani bado ni waaminifu kwa chama licha ya kwamba walipiga kura kinyume na matakwa ya kinara wetu Raila Odinga,” akasema.

You can share this post!

Ni wakati wetu kupata maendeleo, wafoka wabunge wa maeneo...

Wanaomtaka Sancho wamnunue kabla ya Agosti 10 –...

adminleo