• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Maseneta wazidi kutofautiana kuhusu fedha za kaunti

Maseneta wazidi kutofautiana kuhusu fedha za kaunti

Na CHARLES WASONGA

HUENDA maseneta wakakosa kuelewana tena kuhusu mfumo mwafaka wa ugavi wa fedha kwa kaunti, baada ya kamati ya kiufundi iliyobuniwa kusaka muafaka kuhusu suala hilo kukosa kuelewana kuhusu uongozi wake.

Hii ni baada ya maseneta wanaopinga mfumo wa uliopendekezwa na Kamati ya Seneti kuhusu Fedha kupinga uteuzi wa Naibu Spika Profesa Margaret Kamar kuwa mwenyekiti wake.

Maseneta hao maarufu kama, “Team Kenya” jana walidai Profesa Kamar anaendeleza maslahi fulani katika suala hilo, na akipewa uongozi wa kamati hiyo atavuruga ripoti yake.

“Hatuwezi kukubali Naibu Spika Kamar aongoze. Ameonyesha wazi kuwa anaunga mkono pendekezo la kamati ya fedha kwamba kaunti 18 zipunguziwe fedha huku kaunti 29 zikiongezewa,” Kiranja wa Wachache Mutula Kilonzo Junior aliiambia Taifa Leo.

Seneta huyo wa Makueni ndiye kiongozi wa vuguvugu la maseneta wanaounga mkono pendekezo la Seneta wa Nairobi Johnson Sakaja kwamba Sh316.5 bilioni zilizotengewa serikali 47 za kaunti katika bajeti ya mwaka huu.

Kamati hiyo yenye wanachama 10 ilibuniwa Jumatano, siku moja baada ya Seneti kuahirisha mjadala kuhusu suala hilo kusaka muafaka zaidi, kufuatia hoja iliyowasilishwa na Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen.

“Tumeamua kuunda kamati ndogo ambayo itafanya mikutano kwa lengo la kusaka muafaka kuhusu suala hili muhimu,” akasema Bw Lusaka.

Mrengo uliounga mkono mfumo uliopendekezwa na Kamati ya Fedha, inayoongozwa na Seneta wa Kirinyaga Charles Kibiru, jana ulikuwa ulipendekeza maseneta Naomi Shiyonga (Seneta Maalum), Susan Kihika (Nakuru), Ephraim Maina (Nyeri), Samson Cherargei (Nandi) na Ochilo Ayacko (Migori) kuwa wawakilishi wake katika kamati hiyo.

Lakini mrengo unaongozwa na Kilonzo Junior ulidinda kupendekeza wanachama wake usisitiza kuwa hauta kubali uongozi wa Profesa Kamar. Kundi hilo linaunga mkono mfumo uliopendezwa na Bw Sakaja kuwa fedha hizo zigawanywe kwa kuzingatia mfumo wa zamani ambapo hakuna kaunti itakayopoteza.

Kisha fedha nyingine zitakazoongezwa baadaye ndizo zigawanywe kwa kuzingatia mfumo mpya unaotoa kipaumbele kwa kigezo cha idadi ya watu.

Jana, Bw Murkomen alisema “Team Kenya” imemshauri Bw Sakaja kushirikiana na Seneta wa Meru Mithika Linturi ambaye amependekeza marekebisho yao kwa mfumo wake.Bw Linturi anapendekeza kwamba Sh280 bilioni zigawanywe kwa kigezo cha mfumo uliotumika katika mwaka wa kifedha wa 2019/2020.

Baadaye Sh40 bilioni zigawanywe kwa misingi ya matokeo ya sensa ya 2019, ambapo kaunti zenye watu wengi zitafaidi.“Ili kupata suluhu ya mwisho tumemshauri Seneta Sakaja ashirikiane na Seneta Linturi ili watupe ripoti kabla ya Jumatatu Agosti 10.

Tunaamini kuwa muafaka utakaoafikiwa utakomesha majadala kuhusu suala hilo mnamo Jumanne Agosti 11, 2020 Seneti itakapopitisha mfumo utakaokubaliwa na wote,” Murkomen akasema kwenye taarifa kupitia Twitter.

Mnamo Alhamisi, aliyekuwa mwaniaji Urais Petter Kenneth alidai kuwa Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa ODM Raila Odinga wamepanga mikakati ya kukwamua mzozo huo.

You can share this post!

MWANGI: Wanamuziki wakome kudhulumu wapamba ngoma za video

Uhuru amtuma Muraguri kumaliza mzozo mpakani

adminleo