• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 9:50 AM
Washtakiwa kuiba maziwa

Washtakiwa kuiba maziwa

Na RICHARD MUNGUTI

WAFANYAKAZI wakuu katika kampuni ya kutengeneza Maziwa na Chakula ya Highlands walishtakiwa jana kwa wizi wa maziwa iliyo na thamani ya Sh460,000.

Bw Dennis Ndegwa Maina , ambaye ni meneja wa masuala ya teknolojia, Bi Eddah Moraa Ong’ombe ambaye ni meneja katika kituo cha kuuzia maziwa na dereva wa kampuni hiyo Bw Victor Kinara Nyambane walifikishwa katika Mahakama ya Kibera Nairobi.

Walikanusha mashtaka manne mbele ya hakimu mwandamizi Bw Charles Mwaniki Kamau.

Shtaka la kwanza dhidi ya wote watatu ni kwamba kati ya Agosti 1,2019 na Julai 22 mwaka huu jijini Nairobi waliiba maziwa iliyo na thamani ya Sh460,168 mali ya kampuni ya Highlands and Foods Limited.

Shtaka la pili dhidi yao lilikuwa la kula njama za kuiba maziwa hayo.

Shtaka la tatu lilikuwa dhidi ya Eddah na lilisema kuwa mnamo Juni 22 2020 alighushi cheti cha mauzo (LPO) akidai kimetayarishwa na kampuni Game Nairobi.

Pia Eddah alikabiliwa na la kutengeneza bila idhini LPO hiyo akidai limetoka kwa Game Nairobi.

Mawakili watatu wanaowatetea washtakiwa hao waliomba waachiliwe kwa dhamana ya Sh20,000 kama walivyokuwa wamepewa na Polisi.

Kiongozi wa mashtaka Bw George Obiri alipinga wakiachiliwa kwa dhamana ya Sh20,000 akisema mashtaka dhidi yao ni mabaya kwa vile “ walipanga kutekeleza uhalifu huo kwa muda mrefu.”

Aliomba hakimu awaachilie kwa masharti makali ya dhamana.

Akitoa uamuzi hakimu alisema dhamana ni haki ya kila mshukiwa na kuwaamuru kila mmoja alipe dhamana ya pesa tasilimu Sh100,000.

Washtakiwa walilalamika dhamana hiyo iko juu mnamo ikitiliwa maanani walifutwa kazi.

Hakimu aliwashauri washtakiwa hao wawasilishe ombi la kupunguziwa dhamana wakirudi kortini Agosti 31,2020 kesi itakapotajwa.

You can share this post!

Maseneta waunda kikao kingine cha upatanisho

Wanaume wawili kusalia ndani kwa kunajisi mabinti