• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 1:14 PM
Serikali Sudan yatia sahihi mkataba wa maelewano na waasi wa SPLM-N

Serikali Sudan yatia sahihi mkataba wa maelewano na waasi wa SPLM-N

Na MASHIRIKA

KHARTOUM, Sudan

SERIKALI ya mpito ya Sudan imetia sahihi mkataba wa amani na waasi wa Sudan People’s Liberation Movement-North (SPLM-N) ambapo wanachama wa kundi hilo watasajiliwa katika jeshi kufikia Novemba 2023.

Mkataba huo unatarajiwa kumaliza miaka mingi ya ghasia.

Serikali ya mpito ambayo iliingia mamlakani baada ya kupinduliwa kwa dikteta aliyetawala nchi hiyo kwa miaka mingi Omar al-Bashir mwaka jana, imekuwa ikifanya mazungumzo na makundi manne makubwa ya waasi.

Mkataba wake na SPLM-N unahusu majimbo ya Blue Nile na Nuba eneo la South Kordofan, ambapo waasi wamekuwa wakipigana baada ya Sudan Kusini kupata uhuru 2011.

Shirika la habari la serikali la Suna liliripoti kuwa mkataba huo unaweka mipango ya usalama kati ya serikali ya Sudan na SPLM-N.

Pande zote zimekubaliana kundi hilo halitaajiri watoto kuwa wanapiganaji na kwamba halitavuka mipaka ya eneo linalothibiti.

Mkataba huo wa kurasa 50 ulitiwa sahihi Jumatatu katika jiji kuu la Juba, Sudan Kusini na unasema kwamba pande zote zilikubaliana kwamba wapiganaji wa SPLM-N watatoa silaha na kusajiliwa katika jeshi.

Unatambua kwamba mageuzi yaliyotokea Sudan yalitoa nafasi ya kujenga na kujenga jeshi la kitaifa linaloakisi utaifa kwa kushirikisha jamii zote za nchi hiyo.

Serikali ya mpito ya waziri mkuu Abdalla Hamdok imekuwa ikizungumza na makundi ya waasi ikiwemo SPLM-N na yaliyo jimbo la Dafur katika juhudi za kumaliza umwagikaji wa damu wa miaka mingi.

You can share this post!

Biashara ya mitego ya panya na ‘nyumba za kuku’...

Hofu ya mapinduzi baada ya wanajeshi kuzua ghasia Mali