Waziri Mkuu ang'olewa mamlakani Somalia
ABDULKADIR KHALIF na FAUSTINE NGILA
Serikali ya Somalia imemng’oa mamlakani Waziri Mkuu wa nchi hiyo.
Kwenye mswada wa kutokuwa na imani na Waziri huyo uliowasilishwa bungeni Jumamosi, wabunge 170 waliupigia kura.
Spika Mursal Abdulrahman alitangaza matokeo hayobaada ya kufungwa kwa kikao hicho huku akisema
“Kwa kiasi cha wabunge 178 serikali imepoteza kura ya uaminifu kwa wabunge 170.”
Hii inamaanisha kwamba Rais Farmaajo atalazimika kumpiga kalamu Bw Khaire aliyekuwa ofisini kuanzia mwaka Machi 2017.
Bw Khaire ndiye Waziri Mkuu aliyehudumu kwa muda mrefu kutoka Somalia ikomeshe miaka ya vita.
Spika alisema kwamba matokeo hayo yalitokana na serikali kushidwa kufanya uchanguzi uliokuwa ufanyike mwa ka 2020 na kura za urais mwaka 2021.
Rais President Farmaaj alimpongeza waziri huyo Bw Khaire kwa kazi yake ka askasema alkubaliana na maamuzi ya nyuma ya chini..
Alisema kwamba alipendekeza umoja wan chi lakini lazima angetoa idhinisho yake.