Kiini cha vifo vya ngamia si corona, yasema serikali
JACOB WALTER na FAUSTINE NGILA
Vifo vya ngamia vinavyoripotiwa kwenye kaunti za Kaskazini Mashariki haVisababishwi na corona, serikali ilisema Jumatano.
Mkurugenzi wa huduma za mifugo alitoa kauli inayosema kwamba vifo vya ngamia hao vilisababishwa na vidudu vya bakteria inayoleta magonjwa ya kupumua kwenye mifugo.
Serikali ilisema kwenye ripoti kwamba ngamia ambao wameathirika sana ni ngamia wale wa umri wa chini ya miaka miwili kaunti za, Marsabit, Wajir, Isiolo Garissa.
Daktari Ochodo alisema kwamba uchunguzi uliofanywa ulionyesha kwamba vifo hivyo vilisababishwa bakteria.
“Ripoti zinaonyesha kwamba ugonjwa huo unaokuja kwa dalili za kukohoa,kushindwa kupumua,uchafu kwenye ,mapua na kufuatiwa na vifoulihathiri ngamia wachanga.
“Mkurugenzi wa maswala ya mifugo anaweza thibitisha kwamba ugonjwa huo na vifo vya ngamia si corona,” alisema Dkt Ochodo.
Ripoti hizo zilisema kwamba corona ya ngamia ni ugonjwa wa mapua unasambabishwa na virusi.Mara ya kwanza uliripotiwa Saudi Arabia 2012.