Habari Mseto

Pesa za corona kusitishwa Oktoba

August 13th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

 EDWIN MUTAI na FAUSTINE NGILA

Serikali itasimamisha pesa ambazo inawapa watu wa familia ambazo zimeathirika pakubwa na janga la corona mwezi Oktoba.

Waziri wa Leba Samuel Chelugui alisema kwamba malipo hayo yatakamilishwawiki ya kwanza ya oktoba.

Familia 341,958 zimekuwa zikipokea pesa hizo kila wiki ilikuwasaindia wakati huu mgiumu wa janga la corona.

Serikali ilisema kwamba Sh 1.36 bilioni utumwa kwa familia hizo kila mwezi.

Wanaofaidikika na fedha hizo ni watu kutoka mitaa ya mabanda kama Mukuru Kwa Njenga,Mathare,Kibra,Mukuru kwa Reuben Nairobi,Nyalenda Kisumu na Banglandesh Mombasa kati ya mitaa ingine.

Serikali ililenga familia mabazo zina umaskini mwingi zile ambazo ni za wajaane,walemavu au yatima.

Bw Chelugui aliambia wabunge kwamba Sh 10 bilioni zilizotengwa kwa kuwatumia waathiriwa hao zilitumwa kupitia njia ya Mpesa.

Waziri huyo alisema kwamba program hio ililenga familia 699,000 kwenye maeneo bunge 290 katika kaunti 47.

Awamu ya kwanza ililenga kaunti za Nairobi ,Mombasa,Kwale na Kilifi ambazo zilikuwa zimefungiwa ambpo familia 85,300 zilisaindika.