• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 5:10 PM
Wazazi wanaopinga elimu ya kijamii waonywa

Wazazi wanaopinga elimu ya kijamii waonywa

Na Maureen Ongala

KAIMU Kamishna wa Kaunti ya Kilifi, Bw Josephat Mutisya, ameonya wazazi ambao hawatapeleka watoto wao kuhudhuria masomo kupitia mpango wa elimu ya kijamii unaotarajiwa kuanza Septemba 2, wataadhibiwa kisheria.

Akizungumza ofisni mwake, Bw Mutisya alisema kuanzisha kwa mpango ya elimu ya kijamii ni njia moja ya serikali kuwasaidia wanafunzi kupata mafunzo badala ya kuendelea kukaa nyumbani kwa zaidi ya miezi mitano baada ya shule kufungwa kutokana na virusi vya Corona.

“Ni lazima mzazi ambaye anategemea watoto wake kufanya kazi ili wapate pesa ya kununua chakula ajue kwamba ifikapo tarehe mbili mwezi ujao, kila mtoto awe mahali pake pa kusomea kwa saa nne bila kukosa,” akasema.

Kwa sasa, wazee wa mtaa na washirika wa Nyumba Kumi wanaendeleza mikakati ya kuwaorodhesha wanafunzi wote katika vijiji na pia sehemu mbalimbali za mafunzo kaunti hiyo.

Bw Mutisya alieleza watoto wengi wamepotoka wakiwa nyumbani kwa sababu ya kukosa kuwa chini ya uangalifu wa wazazi wao ambao hutoka kila siku asubuhi ili kutafuta riziki.

 

You can share this post!

Young Achievers yaibuka mabingwa

Watu wajilaza kwa majeneza kukabili mahangaiko ya corona