• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Watu wajilaza kwa majeneza kukabili mahangaiko ya corona

Watu wajilaza kwa majeneza kukabili mahangaiko ya corona

Na MASHIRIKA

BAADHI ya watu nchini Japan sasa wanalala ndani ya majeneza ili kusahau mahangaiko yaliyosababishwa na janga la corona.

Kampuni moja ya kuandaa maonyesho ya filamu nchini Japan imeibua mbinu hiyo ya kustaajabisha ya kuondoa wasiwasi kwa kuwahimiza watu walale ndani ya majeneza wanapotizama maonyesho yao ya kutisha yanayohusu vifo na wafu wanaofufuka.

Watu wanahimizwa kulala ndani ya majeneza yenye urefu wa mita mbili na yaliyotengenezwa kwa mbao. Majeneza hayo huwa na madirisha ambayo huwasaidia kusikiza hadithi za kiajabu huku wakitizama filamu hizo.

“Janga hili limesababisha msongo wa kiakili, na tunataraji kuwa watu wanaweza kupata tulizo kidogo kwa kuchangamka na kupiga mayowe,” akasema Kenta Iwana, mshirikishi kwa kampuni hiyo kwa jina “Kowagarasetai” (yaani Kikosi cha Kushtua) ambayo huonyesha filamu za dakika 15.

Huku Japan ikiendelea kuandikisha ongezeko la visa vya maambukiza ya Covid-19, watu 1,034 wakiwa wameambukizwa kufiki Ijumaa, Iwana, 25, anajizatiti kuhakikisha waigizaji wake wanapata kazi.

Kawaida, wao hutumbuiza kwa michezo ya kuigiza katika maeneo kama vile mbuga.“Tamasha nyingi zimefutiliwa mbali kwa sababu ya janga la corona, na nilikuwa nikitafuta njia ya kujiondolea msongo wa kiakili,” akasema Kazushiro Hashiguchi, 36, baada ya kulala kwenye jeneza moja lililogharimu dola 7.60 (Sh760).

“Sasa nahisi nimetulia,” akaongeza.Wateja wanaokuja kutiza sinema hizo, zinazoonyesha katika ukumbi wa mapumziko unaotumiwa na abiria wanaowasili jijini Tokyo wakielekea miji mingine, na wamiliki wa maduka ya kibiashara na wale wanaojihusisha na kazi nyingine.

Iwana anatumai kuwa wamiliki wa majengo mengine watampa nafasi ya kuandaa maonyesho yake ili kuvutia watu wengi.

“Tulihitaji kitu ambacho tunaweza kutembeza kila mahala, na majeneza ni rahisi kuhamisha. Unachohitaji kufanya ni kuyaweka ndani ya chumba ambacho hakina mwangaza,” akasema Iwana.“

Ni biashara nzuri kwetu na inawaridhisha wateja wetu,” akaongeza.Wakati huo huo, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limeelezea matumaini kuwa janga la corona litadhibitiwa kabisa baada ya miaka miwili.

Akiongea jijini hapa Ijumaa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema mlipuko wa homa ya Spanish Flue ya 1918 ilimalizwa baada ya miaka miwili.

Hata hivyo, alisema maendeleo ya sasa katika nyanja ya teknolojia yatawezesha ulimwengu kumaliza virusi vinavyosababisha Covid-19 haraka.

Homa ya Spanish Flu iliua watu milioni 50 lakini kufikia sasa virusi vya corona vimeua karibu watu 800,000 huku watu 22.7 milioni wakiambukizwa.

Tangazo la WHO limejiri siku chache baada ya Uingereza kudai imevumbua chanjo ya kwanza dhidi ya virusi vya corona ambayo ni bora na salama kwa matumizi ya binadamu.

Hata hivyo, mataifa mengi ya ulimwengu yameibua shaka kuhusu chanjo hiyo yakitaka Uingereza kuchapisha mfumo wa kisayansi uliotumika kuitengeneza.

You can share this post!

Wazazi wanaopinga elimu ya kijamii waonywa

Serikali inavyojenga wanasiasa ikidhani inawatia adabu!