• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 12:26 PM
‘Baadhi ya madoli yanaelekeza watoto kujiingiza kwa vitendo vya ngono’

‘Baadhi ya madoli yanaelekeza watoto kujiingiza kwa vitendo vya ngono’

Na MARY WANGARI

MAMLAKA katika Milki ya Falme za Kiarabu (UAE) imewahimiza wazazi kuwa na muda zaidi wa kucheza na watoto wao na kuchukua hatua ya kuhakikisha madoli ya watoto wao yanaambatana na umri wao.

Idara ya Usalama wa Watoto (CSD) inayohusiana na Baraza Kuu kuhusu Masuala ya Familia, Sharjah, ilielezea wasiwasi katika taarifa, kufuatia malalamishi ya baadhi ya wazazi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu jumbe za ngono zinazoelekezwa kwa watoto kupitia aina maarufu ya madoli.

“Idara ya Usalama wa Watoto inatilia maanani malalamishi kutoka kwa kina mama wengi mitandaoni na inatathmini ukweli wake pamoja na mamlaka husika,” amesema Mkurugenzi wa CSD Hanadi Saleh Al Yafei.

Akaongeza: “Tunashirikiana na mashirika husika ya kiserikali kuangazia na kusuluhisha hatari yoyote dhidi ya watoto. Ni sehemu ya jukumu letu kuchukua hatua dhidi ya tishio lolote ambalo huenda likakabili watoto na kutoa uhamasishaji pamoja na suluhisho mwafaka na kushiriki hatua bora.”

Al Yafei amesisitza kuwa usalama wa watoto unaweza kuhatarishwa hasa kupitia vifaa vyao vya kuchezea.

“Watoto wengi huwa na uhusiano wa karibu na vifaa vyao vya kuchezea, hasa wasichana kwa wanasesere wao, maadamu aghalabu hujenga mahusiano ya karibu kwa kucheza na kuwasiliana kana kwamba wanalea. Hii inafanya iwe muhimu hata zaidi kwa wazazi kuhakikisha kwamba vifaa hivyo vinawasilisha ujumbe na maadili mwafaka kwa watoto wao,” akasema Al Yafei.

Alipongeza juhudi za kina mama waliojitokeza kuelezea wasiwasi wao na kuonya wazazi wengine.

“Inapohusu watoto, jukumu huwa zaidi ya wazazi, wajakazi na walimu. Ni jukumu la jamii yote. Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuonya na kutahadharisha wengine dhidi ya hatari zinazoweza kutishia usalama wa watoto kisaikolojia, kimaumbile na hata kijamii,” akaeleza.

You can share this post!

AKILIMALI: Kwake matunda ni tiba na pesa

PSG kupumua baada ya waratibu kusogeza tarehe ya kuanza kwa...