• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 2:10 PM
Familia 28,000 kupokea msaada wa chakula kutoka Base Titanium na serikali ya Mvurya

Familia 28,000 kupokea msaada wa chakula kutoka Base Titanium na serikali ya Mvurya

Na MISHI GONGO

ZAIDI ya familia 28,000 zisizojiweza kutoka eneo la Kinango, Kaunti ya Kwale zimepangiwa kupokea chakula cha msaada kutoka kwa serikali ya kaunti hiyo na kampuni ya kuchimba madini ya Base Titanium.

Kulingana na gavana wa kaunti hiyo Salim Mvurya, familia nyingi katika eneo hilo zinakumbwa na uhaba wa chakula kufuatia mazao yao kukosa kufanya vizuri.

Miongoni mwa vitu watakavyopatiwa ni unga wa ngano, unga wa mahindi, maharagwe, chumvi, na mafuta ya kupikia. Vile vile watapokea sanitaiza na maski.

“Tumekuwa tukishirikiana na washikadau mbalimbali kuwasaidia wakazi wa kaunti hii kupata bidhaa muhimu kujikimu kimaisha. Maisha ya wengi yameathirika kufuatia janga la corona,” akasema gavana huyo.

Wengi wa wakazi wa kaunti hiyo walitegemea sekta ya utalii lakini sekta hiyo ilidorora baada ya kuzuka janga la corona. Wakazi wengi walipoteza ajira.

Aidha aliwatahadharisha wakazi dhidi ya kupuuza masharti yaliyowekwa kudhibiti ugonjwa wa Covid-19.

“Tuendeleeni kuzingatia na kufuata maagizo yaliyowekwa na Wizara ya Afya ili kudhibiti ugonjwa huo,” akasema.

You can share this post!

Kiungo Gareth Barry astaafu soka akiwa na umri wa miaka 39

Sababu 11 Ruto hatajiuzulu