• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Watu 5 wafariki kutokana na corona leo

Watu 5 wafariki kutokana na corona leo

Na CHARLES WASONGA

IDADI ya watu waliofariki kutoka na ugonjwa wa Covid-19 ilikaribia 600 Jumamosi baada ya wagonjwa watano kuangamia ndani ya kipindi cha saa 24 huku idadi ya maambukizi ikiendelea kupungua.

Kufautia vifo hivyo, idadi jumla ya maafa tangu kisa cha kwanza cha ugonjwa huo kiliporipotiwa nchini mnamo Machi 13 imetimu 594. Idadi hii ni sawa na asilimia 1.7 ya idadi jumla ya walioambukizwa virusi vya corona kufikia Jumamosi ambayo ni 35,020.

Kulingana na takwimu zilizotolewa na Wizara ya Afya visa vipya 136 vya maambukizi ya Covid-`19 viligunduliwa Jumamosi baada ya sampuli 3,707 kupimwa ndani ya saa 24.

Kwa mara nyingine, kaunti ya Nairobi ndio iliongozwa kwa kusajili visa 35, Mombasa (25), Kajiado(11), Turkana(9), Kisumu(9), Migori(8), Nyandarua (7), Kilifi(7), Embu (6), Uasin Gishu (4), Busia (3) huku Kisii ikiandikisha visa vitatu vipya.

Baringo, Kakamega, viliripoti visa viwili kila moja huku kaunti za Elgeyo Marakwet, Tharaka Nithi, Kiambu, Kitui and Trans Nzoia zikisajili kisa kimoja, kila moja.

Katika kaunti ya Nairobi idadi kubwa ya visa vilipatikana katika maeneo bunge la Lang’ata, Westlands, Kasarani, Makadara na Starehe

Na katika kaunti ya Mombasa, maambukizi yalikita katika maeneo bunge ya Changamwe, Mvita and Jomvu.

Wagonjwa 99 walipona ndani ya muda wa saa 24, 64 wakiwa ni wale ambao walikuwa wakiuguzwa chini ya mpango wa utunzaji wagonjwa wa Covid-19 nyumbani.

Idadi hiyo inafikisha, 21, 158 idadi ya wagonjwa waliopona kufikia Jumamosi.

You can share this post!

Spika wa Migori apiga ripoti polisi baada ya kutishiwa...

FUNGUKA: ‘Hata na hiki kitambi, sukari ya warembo...