• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 11:55 AM
Sudi ndani kwa siku mbili zaidi

Sudi ndani kwa siku mbili zaidi

RICHARD MAOSI NA JOSEPH OPENDA

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi, amezuiliwa kwa siku mbili zaidi katika kituo cha polisi cha Nakuru Central, akikabiliwa na tuhuma za kutoa matamshi ya uchochezi miongoni ma mashtaka mengine.

Akiwasilishwa na jumla ya mawakili 12, Sudi alikabiliwa na mashtaka tano.

Sudi alijisalimisha katika kituo cha polisi cha Langas police station kaunti ya Uasin Gishu siku ya Jumapili, na hatimaye akasafirishwa kwa ndege hadi Nakuru ambapo alikesha korokoroni, akisubiri kusimama kizimbani.

Kesi yake iliwasilishwa mbele ya hakimu mkuu ,Joseph Kalo kwa njia ya zoom, siku ya Jumatatu ambapo mahakama iliomba azuiliwe kwa siku mbili, ili kutoa muda wa kutosha kukamilisha uchunguzi kabla ya kumshtaki.

Afisa wa Polisi Bw James Akello ambaye anashughulikia mshtakiwa alisema mahakama inapanga kumshtaki Sudi kwa makosa matano, ila wanahitaji muda zaidi kufanya uchunguzi.

Mashataka yanayomkabili Sudi ni yale ya uchochezi,kumiliki silaha bila kibali, kukabiliana na polisi pamoja na kumshambulia afisa wa polisi. PICHA/ RICHARD MAOSI

Afisa huyo aliambia mahakama kuwa polisi walishindwa kumtia mbaroni Sudi usiku wa siku ya Jumamosi, kutokana na idadi kubwa ya wafuasi wake waliojitokeza na kuangusha miti barabarani ili asikamatwe.

Afisa mmoja wa kitengo cha utumishi kwa wote GSU , alipata majeraha katika patashika hiyo.

“Ninatumai mshatakiwa ana habari muhimu ambazo zitasaidia kuharakisha uchunguzi, Isitoshe ufyatuaji wa risasi ulifanya afisa wetu mmoja John Muiruri kupata majeraha,”akasema.

Aidha aliongezea kuwa polisi walipata aina ya bunduki ya Ceska na risasi 11 kutoka kwa Sudi.

Sehemu ya mashtaka ikiongozwa na Daniel Karuri, waliomba mahakama isimpatie mshtakiwa dhamana kwani angehitilafiana na walalamishi.

Karuri aliongezea kuwa mbunge alikuwa na mashataka ya kujibu hususan matamshi ya uchochezi yaliyosababisha hisia kali miongoni mwa wakazi wa eneo lake.

Wakili wake Kipkoech Ngetich alilalamika kuwa mteja wake alikuwa akinyimwa haki ya kikatiba kukatazwa bondi ili aachiliwe huru. PICHA/ RICHARD MAOSI

 

Wakati huo huo kulikuwa na sarakasi wakati ambapo wanaomuunga mkono naibu rais ‘Team Tangatanga’walipoingia katika kituo cha polisi cha Central

Viongozi hao wakiongozwa na mbunge wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen,seneta wa Nakuru Susan Kihika,gavana wa Nandi Stephen Sang na Aisha Jumwa walishinda kituoni siku nzima.

Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri, Hillary Kosgei(Kipkelion) na Nelson Koech wa Belgut pia walihudhuria.

Polisi walifurika ndani na nje ya kituo cha polisi ili kukabiliana na idadi kubwa ya raia waliojitokeza, baadhi wakijaribu kuleta vurugu.

You can share this post!

Fort Jesus yafunguliwa kufufua utalii Pwani

Mwanaharakati ajifunga mnyororo kwenye mnara wa Dedan...