Wasalia bila makao baada ya moto kuchoma nyumba tena
By CHARLES WANYORO
Familia moja Tigania Mashariki kaunti ya Meru imebaki bila makao baada ya moto kutekezeka nyumba yao.
David Nabea na mkewe Sabera Mwari walisema kwamba hii ni mara ya pili kupoteza nyumba kwa kuteketezwa na moto chini ya mwaka mmoja.
Wawili hao walikuwa kazini wakati moto uliteketeza nyumba yao Jumatano.
Mwaka jana familia hiyo ililazimika kuhama baada ya wezi wa mifugo kuvamia nyumbani kwao Thumara na kuchoma nyumba kabla ya kutoroka na mifugo.
“Familia hii ianumia sana na inahitaji usaidizi kwa haraka kutoka kwa wasamaria wema,”a lisema mhubiri Joshua Kiunga.
Moto huo ulitokana na mkulima mmoja aliyekuwa akichoma vichaka uliposambaa na kuharibu mimea huku ukichoma nyumba hiyo ya mbao.
Waathiriwa hao walisema kwamba walipoteza mali ya thamani ya maelfu ya pesa, mavuno na stakabathi muhimu.
Pia, moto huo ulichoma kuku, mbwa na mbuzi waliofungiwa kwenye nyumba.“Tumeachwa bila chochote kwasababu tumeachwa na nguo tulizovaa pekee. Kila kitu kimeteketea,”alisema Bw Nabea.
TAFSIRI, FAUSTINE NGILA