Hasara ya miwa yawasubiri wakulima
Benson Amadala
Wakulima wa miwa Kaunti ya Busia wanakondolea macho hasara baada ya mvua kubwa kuzuia kusafirishwa kwa miwa ambayo tayari walikuwa wamevuna kutoka shambani.
Wakulima ambao wameathirika na ambao husafirisha malighali Busia ni wakulima kutoka kaunti ndogo za Nambale, Malaba na Funyula.
Mvua hiyo imeendelea kwa muda wa wiki mbili huku ikiharibu barabara ambazo zinaeelekea maeneo miwa upatikana.
Viwanja vya miwa vimejaa matope huku ikiathiri usafirishaji wa miwa kwa lori zinazosafirisha miwa kutoka mashambani.
Hii imeelekea kwa visiagi kutafuta vifaa maalum kuvuruta lori lililokwamma kwenye matope na kuathiri usafirishaji wa malighafi kwenye viwanda vya kibinafsi.
Bw Stephen Mula afisa wa mawasiliano kwenye kampuni ya sukari Busia alisema kwamba mvua hiyo imeathiri shughuli za viwanda wa sukari.
“Karibu asilimia 90 ya mashamba yetu ya miwa yako mahala chini na mvua imekuwa changamoto kwa lori kufikia viwanja hivyo ili kusafirisha miwa,” alisema Bw Mula.