Walala nje baada ya nyumba kubomolewa
Na Charles Wanyoro
Familia moja Kaunti ya Meru ililazimika kulala nje wakipigwa na baridi baada ya kikundi cha vijana kubomoa nyumba yao eneo la Kalima Ntiiri kufuatia mzozo wa ardhi.
Vijana hao walitumiwa kubomoa nyumba hiyo kwa niaba ya Bi Kananu Maore huku wamebeba amri ya korti. Nyumba hiyo ilijengwa na Charles Muturia.
Wakili Kirimi Mbogo alisema kwamba walikuwa wanatekeleza amri ya korti iliyopeanwa na Jaji wa Maua Julai 19, 2019 ikimuagiza Bw Muturia kuhama mahali pale.
Bi Kananu alienda korti kuulalamikia kwamba alinunua kipande hicho cha ardhi kutoka kwa Bw Muturia lakini bwana huyo akakataa kuhama mahala hapo.
Bw Muturia badala ya kuhama alijenga nyumba kwenye ardhi hio.
Kananu aliyekasirishwa na hayo alienda kortini ambapo alipewa hati ya kufukuza Bw Muturia.
Kulishuudiwa mvutano huku wanakijiji waliokuwa wamebeba mapanga walikuwa wamesimama karibu wakati vijana hao ambao pia walikuwa wamejihami wakibomoa nyumba hizo za bao.
Bw Mbogo alisema kwamba hali hiyo ilikuwa ya kuogofya kwani polisi walikataa kuwalinda vijana hao waliokuwa wakibomoa nyumba hio.
TAFSIRI: FAUSTINE NGILA