Habari Mseto

Wazee wa Tiriki waomba waruhusiwe kutahiri

August 28th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

Na Derick Luvega

Wazee wa Tiriki wanaiomba serikali kuwaruhusu kuendesha shughuli za kutahiri Oktoba huku vijana 5,000 wakiwa wamewekwa tayari kutahiriwa.

Shughuli hiyo ambayo ilikuwa iendelee Agosti ilisitishwa kwasababu ya janga la corona.

Katibu wa baraza la wazeee wa Tiriki alisema kwamba wako tayari kuzingatia mikakati iliyowekwa na wizara ya afya ili kudhubiti kusambaa kwa virusi vya corona.

“Tukio hilo la kutairi ilisitishwa na wazee,ila wazazi wanasisitiza kwamba Watoto wao watairiwe,” alisema Bw Lipala.

Bw Lipana aliomba serikali iwape vifaa vya kujinga wakitekeleza shughuli hio ya kutahiri.

Wazee wa jamii ya Tiriki huwa na jukumu muhimu katika kupanga ibada hizo muhimu. ufanya kazi muhimu katika sherehe hizo.

Bw Javan Bulemi mwenyekiti wa baraza ya wazee ya Tiriki alisema kwamba janga la corona limeathiri vibaya shugli za kitamanduni.

“Tukio la Kutairi ni moja kati ya matukio makubwa kwenye jamii ya Tiriki.Tukio hilo linaweza simamishwa na magonjwa,janga la njaa ama vita.Virusi vya corona ni kati ya hizo tatu ,”alisema Bw Bulemi wakati shughuli hiyo ilisitishwa Aprili kufuatia kuzuka kwa corona.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA