• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Hakuna vifo vya corona Jumamosi

Hakuna vifo vya corona Jumamosi

Na CHARLES WASONGA

KENYA haikunakili vifo vyovyote kutokana na ugonjwa wa Covid-19 Jumamosi huku visa 105 vipya vya maambukizi vikiripotiwa. Kwa hivyo, idadi jumla ya vifo inasalia 646, ilivyokuwa Ijumaa.

Kulingana na taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Wizara ya Afya, visa hivyo vipya vya maambukizi viligunduliwa baada ya sampuli kutoka kwa watu 2, 868 kupimwa.

Kwa hivyo, kufikia Jumamosi idadi jumla ya visa vya maambukizi nchini tangu Machi 13 ilitimu 36,829. Hii ni baada ya jumla ya sampuli 514,482 kupimwa.

83 miongoni mwa wagonjwa hao wapya ni wanaume ilhali 22 ni wanawake; wote wakiwa na umri kati ya miaka 2 na miaka 75.

Visa hivyo vimesambaa kama ifuatavyo kwa misingi ya kaunti; Nairobi ina visa vipya 33, Busia (15), Mombasa (9), Bungoma (8), Kiambu (4), Nakuru (4), Bomet (4), Garissa (4), Taita Taveta (4) huku  Kajiado ikiandikisha visa vitatu.

Nayo Kakamega kulipatikana wagonjwa wapya watatu, Kisumu (3), Machakos (2), Meru (2), Kitui (2), Trans Nzoia (2) huku  Murang’a, , Nyeri na  Laikipia zikiandikisha kisa kimoja kila moja.

Wizara hiyo inayoongozwa na Waziri Mutahi Kagwe pia imetangaza kuwa wagonjwa 68 wamepona corona. 38 miongoni  mwao ni wale ambao walikuwa wakiuguzwa nyumbani huku 30 walikuwa wamelazwa katika hospitali mbalimbli nchini.

  • Tags

You can share this post!

Mbunge wa Thika azimwa kutoa msaada kwa walemavu

AIBU PUMWANI: NMS yaomba msamaha