Habari Mseto

Madaktari Embu watisha kugoma

September 1st, 2020 Kusoma ni dakika: 1

Na George Munene

Madaktari wa Kaunti ya Embu wametishia kugoma kutokana na mazingira duni ya kufanyia kazi. Walipeana notisi ya siku saba kwa Gavana  Martin Wambora ambaye  walimlaumu kwa kufumbia mahangaiko yao.

Wakiongozwa na katibu wa KMPDU Elvis Mwandiki, zaidi ya madaktari 80 walisema  kwamba hawajapokea mshahara wao wa miezi miwili iliyopita.

Wataalamu hao waliseema kwamba hawajawaipokea marurupu ya corona na walifukuzwa walimokuwa  wakiishi kwasababu ya kutolipa kodi ya nyumba.

Madakatri hao walilia kwamba hakuwa wamelipa kodi ya nyumba na kwamba  wenye nyumba walikuwa wanatishia kuwafukuza.

“Wenzetu wanapitia mambo magumu kwasababu hawajakuwa wakipokea pesa zao,” alisema  Bw Mwandiki.

Waliilaumu pia serikali ya kaunti hiyo kwa kutowapa vifaa vya kujikinga na virusi vya corona.

Madaktari hao waliapa kukatiza shughuli za matibabu kama malalamiko yao hayatashughulikiwa.

Tafsiri na Faustine Ngila