Mawakili waandamana kulalamikia mwenzao aliyeuawa
Na Charles Wanyoro
MAWAKILI wa Kaunti ya Meru wamefanya maandamano mjini Maua kulalamikia kuuawa kwa mwezao Kirimi Mbogo aliyepigwa risasi.
Wanasheria hao waliokuwa zaidi ya 100 waliokuwa wamebeba mabango Jumamosi walifika katika makao makuu ya polisi Igembe Kusini walipohutubiwa na mkuu wa polisi Henry Akongo pamoja na mpelelezi mkuu Samuel Bett.
Baadaye walifika kwenye korti ya Maua na kuzungumza na hakimu mkuu Tito Gesora kabla ya kufika afisini mwa Mbogo walipohutubia wanahabari.
Wakiongozwa na mwenyekiti wa muugano wa baa Meru Ken Muriuki wanasheria kao walizungumzia kuhusu usalama wao na wakaomba uchunguzi ufanyike kwa haraka.
Kesi mingi ambazo zilihitaji uwepo wa mwanasheria huyo chuka,Meru,Maua,Isiolona Nkubu, Meru, Maua, Nkubu and Isiolo zilisitishwa.
Bw Mbogo ambaye alikuwa mwanasheria maarufu alipigwa risasi tumboni Jumatano jioni na mtu aliyekuwa juu ya bodaboda.
Tafsiri na Faustine Ngila