Yaibuka wakili alipigwa risasi kutokana na mzozo wa shamba
Na David Muchui
Chama cha mawakili nchini (LSK) kimesema kwamba kupigwa risasi kwa wakili Kirimi Mbogo Jumatano kulitokana na mzozo wa shamba la ekari 10,000 lililoko Kianda, Igembe Kusini.
Bw Mbogo ambaye alisimamia koo tano zinazodai kumiliki shamba hilo alipigwa risasi nje ya ofisi yake njini Maua kabla ya mhuni huyo kuhepa kwa bodaboda.
Rais wa LSK Nelson Havi aliomba waziri wa Maswala ya Usalama wa Ndani Fred Matiangi kuingililia kati huku akisema kwamba maafisa wa serikali wanahusika na mizozo ambayo imeishi kwa muda mrefu.
Akizungumza akiwa kwenye hospitali ya Kiirua kaunti ya Meru ambapo Bw Mbogo anatibiwa Bw Havi alisema alizungumzia kuhusu kuongezeka kwa maswala ya uhalifu eneo yam lima Kenya na mji waMaua.
“Tunaomba mahakama na mashirika ya serikali kuhakikisha kwamba mizozo ya ardhi imesuluhishwa kwa nia ya kurithisha.Tunajua kwamba Mwanasheria alikuwa anashumgulikia kesi ya ardhi mabyo maafisa wakuu serikalini wanahusika.Wanasheria wanalengwa na walifu ili kuwazima,”alisema Bw Havi.
Tafsiri na Faustine Ngila