• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 12:30 PM
Polisi waanza uchunguzi kuhusu moto uliochoma chuo cha Makerere

Polisi waanza uchunguzi kuhusu moto uliochoma chuo cha Makerere

Na Daily Monitor

Maafisa wa polisi wa nchi jirani ya Uganda wameazisha uchunguzi kubaini ni nini kilichosababisha kuzuka kwa moto ambao umechoma jengo kuu la chuo kikuu cha Makerere.

Kulingana na habari za polisi moto huo unaaminika kuanza Jumapili usiku kwenye paa huku ukisambaa kwenye jengo zima linalowekwa  rekodi za chuo hicho pamoja na idara ya fedha..

“Mali nyingi imeharibiwa. Uchunguzi unaendelea ili kubaini kilisababisha moto huo,” ilisema ripoti ya polisi.

Naibu chanzela wa chuo hicho Profesa Nawangwe alisema kwamba watalijenga tena jumba hilo likae vyenye lilikuwa kitambo kwa wakati mfupi”.

“Nisiku ya kuhuzunisha kwa  chuo kikuu cha Makerere Jengo letu la afisi kuu na usimamizi limeteketea huku vitu mingi zikiharibika,”alisema Prefesa Nawangwe kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter.

Mama wa Taifa wa Uganda Jane Museveni ambaye pia ni Waziri wa Elimu alitarajiwa kufika kwenye eneo la tukio.

Tafsiri na Faustine Ngila

 

  • Tags

You can share this post!

Hospitali nne kusimamiwa na polisi Nairobi

DIGRII ZA MAJUTO: Vibarua licha ya kusoma