• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 6:55 AM
Trump arejea katika ofisi yake ya Oval baada ya huduma za kimatibabu kumsaidia kukabili Covid-19

Trump arejea katika ofisi yake ya Oval baada ya huduma za kimatibabu kumsaidia kukabili Covid-19

Na SAMMY WAWERU na MASHIRIKA

RAIS wa Amerika Donald Trump amerejea katika ofisi ya Oval ilioko katika Ikulu ya White House, chini ya wiki moja baada ya kutangazwa alikuwa akiugua Covid-19.

Trump alitangazwa kuugua corona siku chache baada ya kushiriki mdahalo mkali na mshindani wake mkuu wa kiti cha urais Joe Biden, mjadala walioonekana wakirushiana maneno mazito wakati kila mmoja akinadi sera zake.

Amerika inajiandaa kushiriki uchaguzi mkuu wa urais mwezi ujao, Novemba 3, 2020, Rais Trump akipambana kuhifadhi kiti chake.

Rais huyo alirejea White House Jumatano kwa kishindo, akisema anahisi amepata nafuu na kwamba maambukizi yake ya virusi vya corona yalikuwa ‘baraka kutoka kwa Mungu’ kwa sababu yalileta fursa ya kutumiwa kwa dawa ya majaribio ambayo ni mchanganyiko ya kukabili Covid-19.

“Nimepata nafuu na kurejea, pengine kinga yangu iko juu,” akasema Rais Trump.

Alisema anataka raia wote wa Amerika wapate matibabu aliyopata.

Kwenye video, wakati akirejea kazini, anaonekana akitoa maski na kuhimiza raia wa taifa lake wasiogope corona.

Dkt wake Sean Conley, amesema hajaonyesha dalili za Covid-19 chini ya saa 24 zilizopita na kwamba kiwango chake cha joto kinaashiria kurejea kawaida kwa muda wa siku nne mfululizo.

You can share this post!

Mkutano wa Ruto Kwale wazimwa

Matiang’i apewa mamlaka zaidi ya kudhibiti mikutano...