• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Hofu ya wimbi la pili la maambukizi ya corona

Hofu ya wimbi la pili la maambukizi ya corona

Na CHARLES WASONGA

KWA mara ya kwanza baada ya miezi mitatu, idadi ya visa vya maambukizi ya virusi vya corona nchini ilipanda hadi 604 ndani ya saa 24 na hivyo kufikisha 42,541 idadi ya maambukizi tangu kisa cha kwanza cha ugonjwa huo kugunduliwa nchini.

Nao wagonjwa wengine 10 walithibitishwa kufariki kutokana na Covid-19 katika kipindi hicho na kufikisha 797 idadi ya waliofariki kufikia Jumatano, Oktoba 14, 2020.

Watu hao 604 walipatakana na virusi vya corona baada ya sampuli kutoka kwa watu 5,832 kupimwa; hiyo ni sawa na kima cha maambukizi cha asimilia 10.3..

Kufikia Jumatano, jumla ya sampuli zilikuwa zimepimwa ni 601, 623.

Kwenye taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, hofu ya kuzuka kwa wimbi la pili la maambukizi makubwa kutokana na kile alichosema ni mienendo ya Wakenya kupuuza masharti ya kuzuia kuenea kwa virusi vya corona, imepanda.

Wizara pia ilisema kuwa jumla ya wagonjwa 88 walipona na kuruhusiwa kwenda nyumbani, na hivyo kufikisha 31,428. “56 walikuwa wakitunzwa nyumbani huku 32 ni wale ambao walikuwa wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini Kenya,” Wizara ya Afya ikasema.

Kaunti ya Nairobi ndio iliandikisha idadi ya juu zaidi ya visa vipya vya maambukizi ambapo watu 125 walipatikana na virusi vya corona ikifuatwa na Nakuru yenye visa 113.

Mombasa irekodi visa 87, Busia (35), Uasin Gishu (33), Trans Nzoia (25), Kiambu (25), Kisii (24), Kisumu (24), Kijiado (16) huku Nandi ikiwa na visa 13.

Kakamega ina visa 12 vipya, Meru (11), Machakos (7), Siaya (7) , Garissa (7), Murang’a (5), West Pokot (5), Nyeri (5), Turkana (4), Laikipia (3), Wajir (3), Embu (2), Kirinyaga (2), Narok (2), Marsabi (2), Taita Taveta (2) huku kaunti za Kitui, Nyamira, Tharaka Nithi, Kilifi na  Nyandarua zikiandikisha kisa kimoja kila moja.

You can share this post!

LISHE: Biskuti za viazi vitamu

Jumwa kujibu mashtaka ya mauaji