Kituo cha karantini Mombasa chafungwa
NA SIAGO CECE
Kituo cha kuwatenga wagonjwa wa corona chenye vitanda 300 kaunti ya Mombasa kilichoko kwenye chuo kikuu cha Mombasa kimefungwa kuwaruhusu wanafunzi wa chuo hicho kurejea shuleni.
Kituo hicho cha karantini ndicho kilikuwa kikubwa zaidi kaunti hiyo, na kilianzishwa na gavana wa kaunti hiyo Hassan Joho Aprili ili kuwahudumia wagonjwa wa corona.
Akithibitishwa kufungwa kwa kituo hicho Naibu Chansela wa chuo hicho Abubakar alisema kwamba Zaidi ya vitanda 300 vimetolewa huku chuo hivho kikifungua wiki ijayo.
“Unyunyuzi wa dawa unaendelea huku tukigoja wanafunzi warudi wiki ijayo,”alisema Professa Abubakar.
Kufuatia tangazo la waziri wa Elimu George Magoha wiki iliyopita, wanafunzi wa mwaka wa mwisho wa chuo kikuu na vyuo vya kiufundi wanapaswa kurudi shuleni wiki hii.
Akizungumza na Taifa Leo afisa wa afya wa wa kaunti hiyo Khadija Shikely alisema kwamba wanatafuta nafasi ya wagonjwa wa Corona kwenye hospitali ya Coast general,hospitali ya kaunti ndogo ya Tudor na hospitali yaa Port Reitz.
“Tunataka kujitayarisha kama kutakuwa na maambukizi mengine ya corona. Kulikuwa na wagonjwa wawili pekee waliokuwa wamebaki kwenye kituo hicho,” alisema.
Tafsiri na Faustine Ngila