Habari Mseto

Huzuni wasichana 3 kufa maji bwawani

October 8th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

NA FAUSTINE NGILA

HUZUNI ilitanda Ijumaa katika kijiji cha Mutitu,  Embu baada ya wasichana watatu kufa maji walipokuwa wakiogelea  kwenye bwawa La Kiambere  huku shule zikifunguliwa Jumatatu.

Wasichana hao walikuwwa wanalisha ng’ombe wakati wa kisa hicho. Watatu hao walitambulika kama Cecilia Muthathie wa miaka 12, Nancy Muthoni wa miaka 9 na Jane Ngatha wa miaka 7.

Kulingana na chifu David Muli wawili wa wathiriwa ni wa familia moja. Mashahidi walisema kwamba watatu hao waliwaacha ng’ombe na kuingia kwenye bwawa hilo kuogelea.

Walipokuwa wakiogelea walibebwa na mawimbi ya maji. Wakazi walisema kwamba waliona watoto hao wakijaribu kujiokoa kutoka ndani ya maji hayo na wakajaribu kuwaokoa lakini ikashindikikana.

“Tulijaribu kuwaokoa tuliopoona wakibebwa na maji lakini ilishidikana,” alisema mkazi mmoja. Kufuatia tukio hilo wakazi walianza kutafuta miili ya wasichana hao.

Bw Muli alidhibitisha kwamba miili hiyo ilipelekwa  kwenye chuba cha kuhifadhi maiti cha hospiali ya Embu.

Wazazi waliombwa kuonya Watoto wao kuhusiana na kuogeelea kwenye mabwawa.

“Wazazi wanapswa kuwaonya wanawao kuhusiana na madhara yanayoletwa na kuogelea kwenye bwawa ilikuzuia kupoteza maisha ya Watoto,”alisema.