Habari Mseto

Mafuriko yasomba mtu mmoja Horr, 400 waachwa bila makao

October 11th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

NA JACOB WALTER

Mtu mmoja amefariki na wengine 400 kuachwa bila makao kaunti ndogo ya Horr Kaskazini kufuatia mafuriko yaliyoshuhudiwa eneo hilo Jumamosi jioni.

Mafuriko hayo yalisababishwa na mvua kubwa inayonyesha eneo hilo na dhuruba iliyotokea kwa zaidi ya dakika 30 .

Mzee  mmoja aliripotiwa kufa maji alipokuwa akivuka mto El-boso uliokuwa umefurika wadi ya Turbi.

Chifu wa eneo la Maikona  Guyo Isacko aliambia Taifa Leo kwamba zaidi ya familia 400 zinahitaji chakula,neti za mbu na blanketi baada ya Manyatta zao kkuharibiwa na maji.

“Tunaomba serikali na wasamaria wema wasaindie Zaidi ya familia 400 ambazo zimeachwa bila makao,” alisema Bw Isacko huku  akiogeza kwamba atoto wawili wa mika 5 na 7 wameumia.

Mmoja alivunjika mgu wa kulia huku mwingine akipata majeraha kichwani baada ya kubebwa na maji lakini waliokolewa.

Wawili hao walipelekwa kwenye hospitali ya Kalacha ambapo wamelazwa na wanaendelea vizuri.

Bw Isacko alisema kwamba walioadhirika san ani wanawake Pamoja na Watoto kutoka Manyatta ya Ledhamis ,Dib ana Burji eneo la Maikona huku wakilazimika kuishi kwenye chuo cha ECDE cha Ladhamis na kituo cha afya kilichokokaribu..

Aliogoza kwamba zaidi ya mbuzi 1000 na kondoo walikufa huku akiwaomba waoishi kwenyyee maeneo ya chini wahamie maeneo ya njuu.

Diwani wa Turbi Guyo Diba aliomba serikali na wasamaria wema kuwasaidia waathiriwa hao.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA