Watu sita wahofiwa kufariki Ziwa Victoria
NA VICTOR RABALLA
Watu sita wanahofiwa kuwa walifariki baada ya boti walilokuwa wakisafiria kuzama ndani ya Ziwa Victoria jambo lililotokana na mawimbi na kubeba kupita kiasi Ijumaa usiku.
Ripoti zilisema kwamba watu 13 walikuwa wanatumia boti hilo kusafiri kutoka nchi jirani ya Uganda wakati Lilizama saa nne usiku Budalangi kaunti ya Busia.
Stephen Musee, mwenyekiti wa usimamizi wa ufuoni alisema kwamba boti hilo lilikuwa limetoka kisiwa cha Sigulu Uganda likieleka Sisenye Kenya.
Bw Musee alisema kwamba watu waliokuwa wamepotea ni Waganda watatu na Wakenya Watatuaid the missing people were three Ugandans and three Kenyans.
“Waliokolewa kutokana na janga hilo waliokolewa mapema asubuhi wakiwa wamekwama kwenye boti na gunia zilizokuwa zimeelea njuu ya maji na wavuvi waliokuwa wakitoka kwenye shughuli zao za uvuvi ,’” alisema.
Walipelekwa kwenye hospitali ya Port Victoria na walizi wa ufuoni huku wakianzisha shughlli ya kutafuta miili ya sita hao.
Polisi walitambua waliopotea kuwa Bridget Erumbi, Carol Odimbo , Lucy Odimbo, David Muluka na Evans Okumu na mwenye boti hilo..
Wilkister Ajiambo alisema kwamba aliona mumewe Bw Akuku mara ya mwisho mwezi Agosti.
TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA