Vijana waandamana kumkomesha Ruto kutusi Matiang'i
NA RUTH MBULA
Baadhi ya vijana kutoka kaunti ya Nyamira walifanya maandamano kulalamikia walichosema ni matusi kwa waziri wa Maswala ya Ndani Fred Matiang’i na Naibu Rais William Ruto.
Haya yalijiri saa chache baada ya Naibu Rais kuondoka kaunti hiyo alipokuwa amezuru kwenye hafla ya kuchanga pesa.
Naibu Rais na wafuasi wake waliwakemea maafisa wa serikali ambao walikuwa wanajaribu kusimamisha mkutano yake wiki moja iliyopita
Vijana waomuunga mkono Matiang’i na Rais Uhuru Kenyatta walitaka waziri Matiangi aheshimiwe.
Wakiogozwa na Bi Josephine Nyang’au, kundi hilo la vijana lilisema kwamba linashukuru kwamba naibu Rais anawasaindia vijana lakini wakaomba akome kumtusi waziri Matiangi.
Kundi hilo lavijana lilizungumza na wanahabari Kitutu Masaba waliposema kwamba naibu Raisa anapaswa kuhepukana na viogozi ambao wanamyusi waziri Matiangi.
“Tunataka mtoto wetu aheshimiwe. Hatutaki viongozi ambao wanakuja wakijifanya wanasaindia vijana huku nia yao ikiwa kutusi viongozi wetu,” walisema.
Geoffrey Mose alisema kwamba Naibu Rais anapaswa kujua kwa kumtusi Matiang’i vijana hawawezi kuvutiwa kumpigia kura.
“Hatutaki rukwama, tunataka ajenda lakini si kuhusu Matiang’i. Kiti cha urais hakiwezi kupatikana kwa kuharibia viongozi wengine jina,” waliongeza.
TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA