• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 9:50 AM
Jinsi ya kuandaa kinywaji cha ‘detox’ au kitoa sumu maarufu ‘green juice’

Jinsi ya kuandaa kinywaji cha ‘detox’ au kitoa sumu maarufu ‘green juice’

Na DIANA MUTHEU

[email protected]

NI ndoto ya watu wengi ambao wamekuwa na uzani mwingi kupindukia kuweza kupunguza kilo ili kuimarisha afya zao kwa kufanya mazoezi.

Hata hivyo, mara kwa mara mchakato wa kupunguza uzani hurejeshwa nyuma na aina chakula na vinywaj anavyotumia mtu huyo, licha ya kufanya mazoezi.

‘Detox’ ni mchakato au muda ambao mtu anajinyima vyakula, vinywaji au vitu vingine ambavyo vinaweza kudhuru mwili wake.

Pia, inamaanisha hali ya mtu kula vyakula na kunywa vinywaji vitakavyomsaidia kuondoa vitu vinavyoweza kudhuru mwili wake.

Jinsi ya kuandaa kinywaji cha ‘detox’ au kitoa sumu maarufu ‘green juice’

Muda: Dakika 10

Vinavohitajika

  • tufaha (apple) lenye ukubwa wa wastani
  • tangopepeta (cucumber) ½
  • shina ½ la figili (celery)
  • kipande kidogo cha tangawizi
  • vijiko 2 vikubwa vya juisi ya limau
  • kikombe 1/3 cha maji
  • matawi 4 ya mnanaa (mint leaves) ingawa si lazima
  • dania au fungu 1 la spinachi changa
  • asali
  • blenda
  • kichungi

Jinsi ya kuandaa

Osha viungo vyote ukitumia maji safi.

Ambua ngozi ya tangopepeta, tangawizi na tufaha lako. Toa mbegu katika tufaha, kisha kata liwe vipande vidogovidogo na uvitie katika blenda yako.

Katakata figili yako na uiongeze katika mchanganyo ndani ya blenda.

‘Green juice’ ndani ya blenda. Picha/ Diana Mutheu

Ongeza juisi ya limau, matawi ya mnanaa na asali ndani ya blenda. Saga hadi mchanganyo huo ulainike kabisa.

Kinywaji chako kiko tayari. Waeza kukinywa jinsi kilivyo, au ukitaka ukipitishe katika kichungi ili upate ‘green juice’ laini.

Kinywaji hiki ni bora kikinywewa asubuhi sana kabla ya kula chakula chochote au jioni kabla ya kulala.

Burudika.

You can share this post!

Nema yawaonya wanaomiliki maeneo ya uchimbaji mawe bila...

Walimu wakuu sasa wapinga wanafunzi wote kurejea shuleni