• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 3:55 PM
Wanasayansi watambua sababu ya ndege kukosa meno

Wanasayansi watambua sababu ya ndege kukosa meno

AFP na VALENTINE OBARA

PARIS, UFARANSA

UTAFITI mpya umebainisha kwa nini ndege hawana meno.

Ripoti ya utafiti iliyotolewa Jumatano imeonyesha kuwa ndege hawana meno kwa sababu mayai yao huanguliwa haraka, baada ya siku au wiki chache tu.

Kisayansi, muda zaidi huhitajika ili kiinitete cha kiumbe chochote kile kuumba meno, kwa mujibu wa watafiti Tzu Ruei na Martin Sander kutoka Chuo Kikuu cha Bonn.

Mayai huanguliwa haraka kwa sababu ya hitaji la kuyalinda kutokana na wanyama hatari na majanga ya kimazingira, kwani huwa hayana ulinzi ikilinganishwa na kiinitete cha mamalia kama vile binadamu.

Tafiti za awali zilikuwa zimesema ndege hawana meno kwa sababu midomo yao ina maumbile ya kipekee ya kuwawezesha kudonadona.

Watafiti hao wawili walisema utafiti wao ulibainisha mayai ya dinosaur ilichukua muda mrefu zaidi kabla kuanguliwa, kati ya miezi mitatu na miezi sita, na hivyo basi ndege hao wakubwa walipata muda wa kutosha kuumbiwa meno.

You can share this post!

Wafanyakazi wa serikali wasiofika kazini kukatwa mshahara...

Raila atuzwa kwa kupigania utawala bora

adminleo