Habari Mseto

Polisi aliyemuua wakili kushtakiwa kwa mauaji

October 20th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

NA PIUS MAUNDU

Afisa wa polisi aliyemkata wakili mkono walipokuwa wakizozana mji wa Wote kaunti ya Makueni wiki mbili zilizopita sasa atashtakiwa kwa mauaji, amesema kamanda wa polisi eneo hilo Bw Joseph Napeiyah.

Konstabo Nancy  Njeri wa kituo cha polisi cha Makueni alimvamia mwanasheria huyo kwa panga alipomtembelea kwenye chumba cha kukodisha.

Mwanasheria huyo Onesmus Msaku alifariki Jumapili alipokuwa akitibiwa kwenyee hospitali ya Kenyatta Nairobi.

Bw Napeiyan alisema Jumatatu kwamba alikuwa ameazisha shugli ya kumtoa kazini afisa huyo wa polisi kwenye kituo hicho cha Makueni.

“Uchunguzi umekamilika na mashtaka yake yatabadilishwa kutoka kusababisha majeraha hadi mashtaka aya mauaji,” alisema Bw Napeiyan.

Wawili hao wanasemekana kuwa walikwa wapenzi wa hivyo polisi watachunguza kwamba afisa huyo waa polisi alikuwa analipisha kisasi..

Bi  Njeri amefugiwa kwenye kituo cha polisi cha Makueni alikuwa afikishwe kortini Machakos Jumatatu lakini tareehe hiyo ikasongesshwa hadi  Ijumaa.

“Tumekubaliana kwamba atafikishwa kortini Ijumaa ili kwanza afanyiwe uchunguzi wa kiakili.Tutaakikisha kwamba haki imepatikana,”alisema mwenyekiti wa LSK Kusini Masharriki mwa Kenya.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA